MSIMAMO KATIKA USANIFU MAJENGO NA UJENZI

– Howard Roark anafukuzwa chuo katika chuo cha “Staton Institute of Technology” alipokuwa akisomea fani ya Usanifu Majengo (Architecture).

– Howard Roark alikuwa anaishi nyumbani kwa Mrs. Keating mama yake na Petey Keating ambaye ni schoolmate mwenzake katika Shule ya Usanifu Majengo (School of Architecture), katika chuo cha Staton Institute of Technology.

– Mrs. Keating alikuwa anamuona huruma sana Howard Roard juu ya hatma yake baada ya kufukuzwa chuo kutokana na misimamo yake mikali juu ya fani ya Usanifu Majengo dhidi ya maprofesa wake.

– Mrs. Keating alikuwa anafikiri kwamba ndoto za Howard Roark za kuwa Msanifu Majengo zitakuwa ndio zimekufa baada ya kufukuzwa shule.

– Yeye mwenyewe Howard Roark alikuwa hajali kabisa watu wanamwonaje au kuchukuliaje suala la yeye kufukuzwa chuoni.

– Mrs. Keating anamwambia Howard Roark kwamba Peter mwanaye anahitimu siku hiyo na amefanya vizuri sana darasani hivyo anategemea kwamba anaenda kuwa Msanifu Majengo mashuhuri zaidi Marekani.

– Mrs. Keating anamwambia Howard Roark kwamba Mkuu wa kitivo(Dean) anamwita na pengine anataka kumsaidia hivyo aharakishe kwenda kumuona.

– Howard Roark anaingia ndani lakini anajisahau, mpaka Mrs. Keating anamfuata tena kumkumbusha ndipo anaondoka.

– Howard Roark ana staili yake ya kipekee ya kufanya Ubunifu katika majengo, pamoja namna ya kipekee ya kupangilia vipengele muhimu katika jengo vinavyolipa jengo utambulisho fulani wa muundo na zama ambazo jengo hilo linajitambulisha nayo au mchanganyiko wa zama.

– Howard Roark hajali sana kuhusu kuenzi zama zilizopita hivyo majengo yake sio ya staili ya Classical greek period( Zama za Ugiriki ya kale), wala Gothic style, wala Renaissance style bali ni Howard Roark style ya kipekee kabisa.

– Misimamo yake hii ndio imemuweka kwenye matatizo mpaka kufukuzwa katika shule ya Usanifu Majengo.

– Howard Roark anaenda kuonana na mkuu wa kitivo(Dean) kujadili suala kufukuzwa kwake.

– Mkuu huyo wa kitivo(Dean) anamwambia Howard Roark, kwamba hakupiga kura ya yeye kufukuzwa chuo bali ni kati ya waliojaribu kumtetea.

– Anamwambia pia kwamba Profesa wake wa Structural engineering(Uhandisi mihimili) na Profesa wake Mathematics(Hisabati) wamejaribu kumtetea sana asifukuzwe chuo.

– Lakini Profesa wake wa kukosoa Ubunifu wa majengo alitishia kwamba endapo Howard Roark hatufukuzwa chuo hicho yeye atajiuzulu kazi.

– Hivyo mkuu kitivo(Dean) anamwambia Howard Roark kwamba atakuwa amemuudhi sana Profesa huyo, Howard Roark akasema ndio.

– Mkuu wa kitivo(Dean) anajaribu kumshawishi Howard Roark kubadili misimamo yake na kujaribu kuhakikisha kazi zake zinakuwa na mwendelezo wa staili za zamani ili ziweze kukubalika na watu hususan watu mashuhuri na watu wa ndani ya fani.

– Howard Roark anasema yeye haoni kwa nini afuate mkumbo tu bila kuangalia sababu za msingi za yeye kufanya hivyo. Howard anasema staili nyingi za zamani za majengo anazolazimishwa kuendana nazo ni staili zilizopitwa na wakati kwa sababu zilifanyika hivyo kutokana na maana na teknolojia ya wakati ule, kuiiga moja kwa moja na kulazimishia iendane na wakati wa sasa wenye teknolojia tofauti ni kushindwa kufikiria.

GOTHIC ARCHITECTURE.

– Mkuu wa kitivo(Dean) anamwambia Howard Roark akumbuke kwamba anaenda kutoa huduma ya usanifu Majengo kwa wateja huko mtaani, hivyo anafikiri ni nani atamruhusu kufanya anachotakiwa yeye?

– Howard Roark anamwambia Dean asiulize kuwa ni nani atamruhusu bali aulize ni nani atamzuia.

– Howard Roark anasema wapo wateja watakaokubaliana naye na hao ndio atakaowahudumia kwani kazi yake ni kutoa huduma bora sana kwa mteja na kumweleza ubora na umuhimu wake.

RENAISSANCE ARCHITECTURE

– Dean anamwambia Howard Roark hashauriki na haoni kama kuna haja ya kuendelea kumshawishi. Howard Roark naye anasema hahitaji tena kuendelea na shule hapo na hawezi kubadilika kuendana na kile ambacho hakiamini wala hakimfurahishi.

– Howard Roark anakutana na Peter akiwa mwenye furaha sana baada ya kuhitimu masomo yake ya Usanifu Majengo kwa matokeo makubwa sana na kusifiwa sana huku akiwa amepewa ofa mbili, moja ni kazi ya moja kwa moja kwenye kampuni kubwa sana ya Usanifu Majengo Marekani na mbili ni Ufadhili wa kuendelea na masomo huko Ufaransa.

MODERN UNIQUE ARCHITECTURE.

– Mama yake Peter ambaye Mrs. Keating anajivunia sana mafanikio haya ya Peter.

– Lakini Peter anashindwa kufanya maamuzi ya afanye chaguo gani kati ya hayo mawili. Hivyo Peter anamwomba Howard Roark amsaidie kuamua kati ya machaguo hayo.

– Peter anamwamini sana Howard Roark kuliko mtu yeyote, kuliko hata maprofesa wake wa chuo.

– Howard Roark anamwambia Peter anatakiwa afanye maamuzi mwenyewe kwani hafikiri kama kuna mtu wa kumsaidia juu ya hilo.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *