HOWARD ROARK ANAFANYA KAZI KWENYE KAMPUNI YA GUY FRANCON

KITABU: FOUNTAINHEAD.

AUTHOR: AYN RAND.

– Howard Roark anatembelea kwenye maeneo ya ujenzi kufanya ukaguzi kutokea kwenye kampuni ya Francon & Heyer.

– Howard Roark anavutiwa zaidi na kazi za site kuliko kazi za ofisini.

– Howard Roark wanakutana na Mike kwenye eneo la ujenzi akifanya ukaguzi na wanaelewana. Wanakaribishana chakula cha jioni na vinywaji.

– Peter Keating anaelekea Washington kwa ajili ya kusimama ujenzi wa mradi mkubwa wa Makumbusho ambao umefadhiliwa na mtoa misaada ambaye ni tajiri sana.

– Guy Francon anamwita Howard Roark na kumwambia kwamba kuna mteja anahitaji kufanyiwa kazi nzuri lakini anahitaji ifanyike vile anavyotaka yeye. Hivyo anamtaka Howard Roark amsikilize na kumfanyia kazi vile anavyotaka yeye.

– Howard Roark anasikiliza maelekezo kutoka kwa Guy Francon. Lakini Howard Roark anakataa maelezo yake na kuanza kumpa maelekezo yeye. Guy Francon anakasirika na kumfukuza kazi.

– Howard Roark anatafuta kazi kwenye makampuni mbalimbali lakini anakosa. Howard Roark anagundua kwamba mambo yake yanafahamika. Kila ofisi aliyoenda anakuta anajulikana kwamba alifukuzwa chuoni Stanton na amefukuzwa pia kazi kwenye kampuni ya Francon & Heyer na Guy Francon.

– Kwa hiyo ofisi hizo kwa kugundua kwamba Howard Roark amefukuzwa kwenye kampuni nyingine na alifukuzwa chuo pia zinagoma kumwajiri kwa kujua kwamba atakuwa ni mtu mwenye changamoto zaidi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *