USANIFU MAJENGO NA UJENZI – 11

KITABU: FOUNTAINHEAD.

AUTHOR: AYN RAND.

1. Howard Roark ameenda kufanya kazi ya kibarua kwenye kiwanda cha Guy Francon cha kupasua mawe huko Connecticut.

2. Dominique ameenda mapumzikoni huko Connecticut kwenye estate hoteli ya kifahari ya baba yake ambayo haiko mbali na kiwanda hicho cha kupasua mawe.

3. Dominique anatembelea kiwanda hicho na kumuona Howard Roark akifanya kazi hiyo ya kibarua, akipasua mawe. Ghafla Dominique anavutiwa sana na Howard Roark ambaye anamuona kama ni wa kipekee sana.

4. Dominique anamwangalia sana Howard anajikuta akifurahia sana kumwangalia vile anavyofanya kazi. Wanaangaliana na kushangaana mara kwa mara bila kuongea chochote.

5. Dominique anarudi mara kwa mara na kumwangalia Howard Roark. Mwisho anaamua kuvunja ukimya na kumuuliza, “kwa nini kila mara unaniangalia sana”, Howard Roark akamjibu, “kwa sababu hiyo hiyo ambayo wewe unaniangalia sana”. Dominique anamwambia mbona anamjibu jeuri, anaweza kumfukuza kazi muda wowote. Howard Roark anamjibu ni sawa.

6. Dominique anajikuta akijitahidi kujizuia asiende kumwona Howard Roark, lakini hilo linakuwa ni gumu sana kwake. Mara kwa mara anajikuta ameshakwenda kumuona.

7. Dominique anaenda mgodini/kiwandani na kumwambia Howard Roark aende nyumbani kwake akamsaidie kazi ya kurekebisha marble tile iliyoharibika na kwamba atamlipa kwa saa. Howard Roark anaenda nyumbani kwenye chumba cha hoteli cha Dominique na kufanya marekebisho hayo kisha kuagiza marble tile iliyokosekana huku wakizungumza mambo mengi na kisha kuondoka.

8. Dominique anasubiria kwa hamu hiyo marble tile ifike ili Howard Roark aje kui-fix lakini baada ya marble kufika baada ya siku chache anaagizwa mtu mwingine kutokea pale mgodini kuja kuiweka na sio Howard Roark.

9. Dominique anaendelea kumfikiria sana Howard Roark ambaye hajamuona kwa muda mrefu kwa sababu hajatembelea hapo kiwandani.

10. Siku moja Howard Roark anakuja moja kwa moja mpaka nyumbani kwenye chumba cha hoteli cha Dominique. Wanaangaliana kwa muda mrefu Dominique akiwa kitandani bila kuongea chochote. Ghafla Dominique anaruka kutoka kitandani na kumfuata wanakumbatiana na baada ya muda wanafanya mapenzi. Kisha Howard Roark anaondoka chumbani kwa Dominique bila kufanya chochote.

11. Baada ya siku chache Howard Roark anapokea barua ambayo inamfikia kupitia rafiki yake Mike aliyeko New York kutoka kwa Roger Enrique.

12. Roger Enrique ameona kazi iliyofanywa na Howard Roark ya John Fargo na kuvutiwa nayo na hivyo anahitaji huduma yake.

13. Howard Roark anaondoka mara moja Connecticut kwa treni kwenda New York.

14. Kwa muda mrefu mrefu Dominique hajamuona Howard Roark na hivyo alikuwa anatamani sana amuone. Dominique akajaribu kwenda kule mgodini kumtafuta Howard Roark bila mafanikio, alizunguka kila eneo la kiwanda lakini hakumuona.

15. Dominique anaamua kumuuliza msimamizi wa ufundi alipo Howard Roark hajui jina lake lakini anamtaja kama mtu mwenye nywele nyekundu. Msimamizi huyo wa ufundi anamjibu kwamba aliondoka jana yake kwenda New York.

16. Dominique anafikiri lakini anaamua kutouliza jina lake. Dominique anaamini kwamba asipojua jina lake atakuwa huru dhidi yake. Anajua hawezi kwenda New York kumuulizia kibarua asiye na jina. Lakini anajua akifahamu tu jina lake ataenda kumuulizia New York na akimpata atapoteza uhuru wake. Hivyo Dominique anajizuia kabisa kufahamu jina lake ili awe huru dhidi yake.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *