USANIFU MAJENGO, UJENZI NA MAPENZI – 13

KITABU: FOUNTAINHEAD.

AUTHOR: AYN RAND.

1. Roger Enright ana biashara nyingi na ana mafanikio makubwa sana. Alipambana sana mwenyewe kufikia mafanikio hayo bila msaada wa mtu yeyote. Ni mtu mwenye misimamo yake na sio mtu wa kujali sana kuhusu watu wanasemaje kuhusiana naye. Watu wengi wanamchukia kwa utajiri wake na hata baadhi ya matajiri wanamchukia kwa namna anavyoishi maisha yake kipekee.

2. Roger Enright anatumia miezi sita kutafuta mtaalamu wa Usanifu Majengo kwa ajili ya jengo lake.

3. Mwisho Roger Enright anampa Howard Roark kazi hiyo baada ya kufanya naye mahojiano kwa muda wa nusu saa.

4. Howard Roark anafungua upya ofisi yake aliyokuwa ameifunga kwa sababu ya madeni na kuajiri wafanyakazi kadhaa wa kumsaidia kazi za michoro.

5. Howard Roark anafanya kazi sana na akili yake yote anaiweka kwenye kazi kiasi kwamba kuna wakati analala ofisini akifanya kazi.

6. Howard Roark hamfikirii Dominique mara kwa mara lakini anapata hisia kali anapomkumbuka. Anajua anapoweza kumpata Dominique lakini hahangaiki kumtafuta, anaamua kusubiri kwanza.

7. Austen Heller anamshawishi Howard Roark kuhudhuria kwenye sherehe iliyoandaliwa na Mrs. Ralston Holcombe maarufu kama Kiki Holcombe. Howard Roark anamkatalia na kuhoji ina umuhimu gani.

8. Austen Heller anamshawishi kwamba ni sherehe muhimu sana na ameambiwa aje na mtaalamu aliyefanya kazi ya Roger Enright na amewaahidi kwamba atamleta. Anaendelea kumshawishi lakini Howard Roark haonekani kukubaliana naye.

9. Austen Heller anaendelea kumshawishi kwamba atapata nafasi ya kukutana na Joe Suttan na hivyo kujenga ushawishi wa kupata mradi wake mkubwa sana. Anamshawishi kwamba atakutana na watu wengine mashuhuri kama vile John Erik Snyte, Peter Keating, Guy Francon na binti wa Guy Francon ambaye ni Dominique ambaye mwandishi mashuhuri wa makala za majengo zinazosomwa sana ambapo ni muhimu akakutana naye.

10. Howard Roark anaposikia kwamba Dominique anahudhuria anashtuka na kupata shauku ya kuhudhuria. Hivyo anamkubalia Austen Heller kwamba lazima atahudhuria.

11. Howard Roark na Austen Heller wanafika kwenye sherehe na Heller anamtambulisha Roark kwa Kiki Holcombe ambaye alitamani sana kumwona Howard Roark na kusifia kazi yake ya nyumba ya Roger Enright.

12. Heller anamtambulisha Howard Roark kwa Dominique na kuwaacha wakiongea mpaka John Erik Snyte anatokea na kuwaingilia na kumchukua Howard Roark kuzungumza naye.

13. Howard Roark anatambulishwa kwa watu wengi sana mashuhuri na kuzungumza nao. Anatambulishwa kwa kazi yake maarufu ya jengo la Roger Enright.

14. Ellsworth Toohey, Dominique na Kiki Holcombe wanakuwa na mjadala mkubwa wa kuhusu falsafa.

15. Kesho yake Ellsworth Toohey anaenda ofisini kwa Dominique, anajaribu kumshawishi kwamba Peter Keating ana uwezo mkubwa kuliko Howard Roark. Anamwambia kwamba Howard Roark alifukuzwa kwenye shule ya Usanifu majengo na hakuweza kumaliza wakati Peter Keating alimaliza akiwa mwanafunzi bora wa darasa lao walilokuwa wanasoma na Howard Roark. Anamwambia pia Peter Keating anafanya kazi kwenye kampuni ya baba yake kwa mafanikio wakati Howard Roark alifukuzwa kwenye kampuni hiyo, na kwamba Peter Keating ni maarufu na amefanya miradi mingi mikubwa kama ule wa Cosmo-Slotnick wakati Howard Roark hajafanya miradi mikubwa ya ujenzi.

16. Dominique anashindwa kumvumilia Ellsworth Toohey na kumfukuza ofisini kwake.

17. Joe Sutton anaenda kuomba ushauri kwa Dominique juu ya mtaalamu sahihi wa kumtumia kwenye jengo lake, wanajadili kwa muda mrefu na Joe Sutton anaamua kwamba hatamtumia Howard Roark.

18. Dominique anaenda kwa Howard Roark na kuingia moja kwa moja kama vile ni mwenyeji wa hapo. Howard Roark anamuuliza amefuata nini, Dominique anamjibu, unajua nilichokifuata. Howard Roark anamwambia ni sawa lakini nataka nisikia ukisema kwa maneno yako. Dominique anamwambia nataka kulala na wewe. Hapo wanafanya mapenzi kisha wanaanza kuongea.

19. Dominique anamwambia Howard Roark anajua kwamba anamchukia na anataka kumwangaza na kitendo cha kulala naye ni sehemu ya mikakati hiyo. Howard Roark anacheka na kumwambia ni sawa.

20. Dominique anamuuliza Howard Roark kwa nini alikuwa anafanya kazi ya kupasua mawe kule Connecticut kwenye migodi ya baba yake wakati ana taaluma kubwa na angeweza kufanya kazi kwenye ofisi yoyote ya Usanifu Majengo hapo New York. Howard Roark anamjibu kwamba kama angefanya hivyo asingepata nafasi hiyo ya kumwangamiza.

21. Howard Roark na Dominique wameendelea kukutana mara kwa mara lakini hakuna mtu hapo New York amefahamu kuhusu mahusiano yao.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *