USANIFU MAJENGO NA UJENZI, UJENZI WA HEKALU – 14

KITABU: FOUNTAINHEAD.

AUTHOR: AYN RAND.

1. Ellsworth Toohey alikuwa ni mwanafunzi bora hasa kwenye masomo ya falsafa tangu anasoma shule msingi. Alichaguliwa kwenda chuo kikuu cha Harvard akasomea digrii ya masuala ya sanaa japo shangazi ambaye ndiye alikuwa mlezi wake baada ya mama yake kufariki alitamani asomee Uchumi akiamini angepata kazi nzuri zaidi.

2. Ellsworth Toohey alikuwa kijana mwenye ushawishi mkubwa shuleni na vyuoni na watu wengi walimpenda na kumfuata na vijana wadogo walimwona kama role model wao.

3. Ellsworth Toohey anasimama na falsafa ya kwamba mtu anapaswa kufanya vitu kwa faida ya watu badala ya kuwa mbinafsi. Pia alichukia sana majivuno na kuhesabu majivuno kuwa ni uovu mkubwa.

4. Ellsworth Toohey anafanya kazi kwenye kampuni ya magazeti ya Gail Wynand na amepewa uhuru wa kuandika chochote anachotaka. Ni mkosoaji mkubwa wa fani ya Usanifu Majengo na pia mara nyingi hachukui mshahara.

5. Jengo la Roger Enright linafunguliwa rasmi huku wakihudhuria watu wachache sana kwani Enright mwenyewe hakuhitaji kuhudhuriwa kwa watu wengi japo alikuwepo mpiga picha, Howard Roark mwenyewe na baadhi ambao hawakualikwa.

6. Jengo hilo linapata wapangaji kwa haraka sana, lakini licha ya kwamba wapangaji hao hawaelewi falsafa iliyotumika kufanya jengo hilo hata hivyo wanafurahia sana maisha katika jengo hilo.

7. Baadhi ya wafuasi wa Ellsworth Toohey ambao ni wanafunzi wanajaribu kumwandikia kumtaka Ellsworth Toohey azungumzie jengo hilo la Roger Enright lililofanywa na Howard Roark katika makala zake. Ellsworth Toohey anajibu kwa ujumbe binafsi kwamba kuna majengo muhimu makubwa duniani ya kuzungumzia hivyo hawezi kuwa na muda wa kuzungumzia jengo lisilo na umuhimu wowote.

8. Howard Roark anakuza ofisi yake kufikia kuwa na vyumba vinne vya ofisi na kuongeza wafanyakazi wasaidizi. Vigezo vya mtu kufanya kazi kwenye ofisi yake ni uwezo na ni mara chache sana hujikuta ameajiri mtu asiye na uwezo ambapo kwa kawaida hawezi kudumu kwenye ofisi hiyo kwa zaidi ya mwezi mmoja. Muda wote yuko busy na kazi na hana biashara nyingine ofisini kwake au na wafanyakazi wake zaidi ya kazi.

9. Kent Lansing anataka kumpa Howard Roark kazi ya kufanya jengo kubwa la kampuni yake linalokwenda kujulikana kama Aquitania hotel. Hata hivyo bodi ya wakurugenzi inamkataa Howard Roark. Kent Lansing anapambana kuishawishi na kulazimisha sana mpaka Howard Roark anafanikiwa kupewa kazi hiyo.

10. Dominique na Howard Roark bado wako kwenye mahusiano ya kina sana ya kimapenzi. Mara kwa mara Dominique anaenda nyumbani kwa Howard Roark na mara nyingine wanaenda nje ya mji lakini bado mahusiano yao hayajawa wazi kwa mtu.

11. Ellsworth Toohey anajaribu kupambana kuzuia mradi wa Aquitania hotel asipewe Howard Roark lakini bila mafanikio. Dominique anamtembelea ofisini kwake kwa mara ya kwanza na kumwambia kwamba anajua kwamba anafahamu alikuwa hataki mradi wa Aquitania apewe Howard Roark, lakini yeye binafsi Dominique amefurahi sana na amempenda sana Kent Lansing kwa kumpa mradi huo Howard Roark. Ellsworth Toohey anamwambia Dominique anakosea sana.

12. Hopton Stoddard ni tajiri mkubwa. Ni mmoja kati ya watu wanaomsikiliza sana Ellsworth Toohey na kuvutiwa naye sana kwa mambo mengi isipokuwa anapata ukakasi kwenye eneo la kwamba Ellsworth Toohey haamini Mungu.

13. Hopton Stoddard anataka kujenga hekalu kubwa kwa ajili ya watu kumwabudu Mungu. Anamshirikisha Ellsworth Toohey lakini Toohey anampinga juu ya wazo hilo na kujaribu kumshawishi ajenge shule kwa ajili ya watoto wenye ulemavu. Hopton Stoddard anajisikia vibaya kutolewana na Ellsworth Toohey kwa sababu anamheshimu sana na kumsikiliza. Hivyo Hopton Stoddard anapata wakati mgumu sana na kuahirisha mradi huo wa hekalu kwa muda.

14. Baadaye Ellsworth Toohey anamfuata Hopton Stoddard na kumwambia yuko sahihi kabisa juu ya wazo lake la kujenga hekalu na yeye ndiye alikosea. Hopton Stoddard anafurahi na kujisikia vizuri sana, haamini kwamba anaweza kuwa amekuwa sahihi kumzidi Ellsworth Toohey ambaye anamwamini sana.

15. Sasa Hopton Stoddard na Ellsworth Toohey wamekubaliana kwamba hekalu hilo litajengwa. Hopton Stoddard anamwambia Ellsworth Toohey kwamba anamsikiliza kwa kila kitu, yeye ndiye atakuwa anaamua chochote.

16. Ellsworth Toohey anamwambia ni sawa na wanatakiwa kuanza kwa kuchagua mtaalamu sahihi wa kufanya kazi hiyo.

17. Ellsworth Toohey anamwambia Hopton Stoddard kwamba mtaalamu sahihi wa kufanya kazi hiyo ni Howard Roark. Lakini anamtahadharisha kwamba Howard Roark ni mtu mwenye misimamo na kama hukubaliani naye anaweza kugoma kufanya. Hivyo anatakiwa kuwa naye makini sana kwenye makubaliano.

18. Ellsworth Toohey anamwambia Hopton Stoddard kwamba pia kwa sababu ni hekalu huenda Howard Roark akakataa kufanya kwa madai kwamba haamini Mungu lakini asimsikilize juu ya hilo kwani Howard Roark ni mtu wa dini sana na hilo linaonekana wazi kwenye majengo yake. Ellsworth Toohey alimpa Hopton Stoddard ujanja mwingi wa kuweza kumshawishi Howard Roark kufanya kazi hiyo lakini akampa tahadhari kwamba asije akamtaja Ellsworth Toohey kwamba ndiye amempendekeza kwamba. Ellsworth Toohey alitaka Hopton Stoddard aape kabisa kwamba hatamtaja.

19. Ellsworth Toohey anatoa sababu kwamba ana marafiki wengi wasanifu majengo na hivyo ikijulikana kwamba yeye ndiye alimpendekeza Howard Roark kwamba mradi muhimu kama huo hawatajisikia vizuri na hapendi kuwaumiza hivyo Hopton Stoddard akaweza kuelewa.

20. Howard Roark alifika ofisini kwa Hopton Stoddard na baada ya kumweleza kweli Howard Roark alisema hataweza kufanya kazi hiyo kwa sababu yeye mwenyewe haamini Mungu. Hopton Stoddard aliposikia hivyo alifurahi na kuzidi kumkubali Ellsworth Toohey kwa kuona kwamba yote ambayo Ellsworth Toohey alikwambia kuhusu Howard Roark yanatimia na kuona kwamba atafanikiwa kumshawishi.

21. Hopton Stoddard anamwambia Howard Roark kwamba amefuatilia kazi zake na kujiridhisha kwamba yeye ni mtu wa dini sana hivyo anaamini anaweza kufanya kazi hiyo ya hekalu. Anamwambia yeye afanye tu hekalu la mambo ya kiroho hata kumi ni kwa roho za watu lakini hekalu kwa yoyote ambayo yeye anaona anafaa. Howard Roark anaelewa lengo la Hopton Stoddard na kukubali kufanya kazi hiyo.

22. Jengo la Cosmo-Slotnick linafunguliwa rasmi na watu wengi wanahudhuria akiwemo Ellsworth Toohey na Peter Keating. Ellsworth Toohey anampongeza Peter Keating kwa kufanikisha kazi hiyo. Tukio zima linatangazwa sana kwenye vyombo vya habari.

23. Howard Roark anaanza kazi ya kufanya design ya jengo la hekalu la Hopton Stoddard. Anamtafuta Steven Mallory kwa ajili ya kazi ya kuchonga sanamu itakayokuwa sehemu ya hekalu hilo.

24. Anapata shida kumpata Steven Mallory lakini mwisho anafanikiwa kufika nyumbani kwake na kumkuta. Steven Mallory anataka kujua kwa nini Howard Roark amemtafuta yeye kwa kazi hiyo akihisi kwamba labda kuna namna anataka kunufaika naye na Howard Roark anamwambia ni kwa sababu ana uwezo.

25. Steven Mallory wanazungumza sana na Howard Roark kiasi kwamba Howard Roark anamuuliza kwa nini alitaka kumuua Ellsworth Toohey. Hata hivyo anamwambia kama hajisikii kujibu sio lazima ajibu lakini Steven Mallory anamwambia ni swali muhimu.

26. Jengo la Aquitania hotel linasimama kwa kuwa wamiliki wake wamefilisika na wengine kuwa na kesi mahakamani. Ellsworth Toohey analiita “Unfinished Symphony” na Dominique analiandika namna hiyo kwenye makala zake.

27. Howard Roark na Steven Mallory wanajadiliana juu ya mwanamke sahihi atakayekaa uchi ili sanamu ya kwenye hekalu ichongwe kwa mfano wake na wanapata changamoto ya kumpata mtu sahihi. Howard Roark anajaribu kumtaja Dominique na Steven Mallory anasema huyo angefaa sana lakini hawezi kukubali. Wanajaribu kumgusia na Dominique anakubali.

28. Ellsworth Toohey anasikitika na kumwambia Dominique hajafurahia yeye kuchongwa sanamu ya uchi ya kukaa kwenye hekalu. Peterson Keating naye anapinga na kumwambia Dominique kwamba hafurahii hata ukaribu wake na Howard Roark. Anamwambia yuko tayari kumwona ana ukaribu na mtu yeyote isipokuwa tu Howard Roark.

29. Dominique anaendelea na mpango huo na anakaa uchi kwenye eneo hilo la hekalu mbele ya Steven Mallory na Howard Roark ili sanamu hiyo ichongwe kwa mfano wake. Wakati wote huo eneo la hekalu limezungushiwa uzio kiasi kwamba hakuna aliyekuwa anaona kinachoendelea ndani ya eneo la ujenzi.

30. Kazi ya ujenzi wa hekalu inaendelea na hekalu linakamilika.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *