USANIFU MAJENGO NA UJENZI – 26 MIRADI ZAIDI YA UJENZI

KITABU: FOUNTAINHEAD.

AUTHOR: AYN RAND.

1. Peter Keating anaenda ofisini kwa Howard Roark kujaribu kumshawishi amsaidia kufanya kazi hiyo ya mradi wa serikali wa Cordlandt wa watu wa kipato cha chini.

2. Howard Roark anamwambia yuko tayari kufanya hivyo lakini kwa masharti fulani. Peter Keating anamuuliza kama yeye hahitaji mradi huo anamjibu kwamba anahitaji lakini hawezi kuendana na miradi ya serikali hususan chini ya ushawishi wa Ellsworth Toohey.

3. Peter Keating anamwambia Howard Roark kwamba yuko tayari kufanya chochote ili amsaidie katika kazi hiyo.

4. Howard Roark anamwambia aende kwanza nyumbani akafikirie kisha waonane kesho yake wazungumzie mradi huo wa Cordlandt.

5. Siku iliyofuata wanakutana na Howard Roark akamuuliza Peter Keating kama yuko tayari kukubaliana na masharti yake. Peter Keating anamwambia yuko tayari kukubaliana na kitu chochote hata ikiwa ni kuuza roho yake yuko tayari.

6. Howard Roark anamtaka Peter Keating ampe sababu ya kwa nini anafikiri anahitaji kumsaidia kwenye mradi huo wa Cordlandt. Anamwambia amwambie kwa nini na anaahidi nini. Wala hamfanyii bure bali kila upande unafaidika.

7. Peter Keating anamwambia Howard Roark atachukua pesa zote za mradi peke yake. Howard Roark anamwambia hilo haliwezi kumshawishi.

8. Peter Keating anamwambia akifanya hivyo atakuwa amuokoa sana, Howard Roark anamwambia amwambie sababu ya kwa nini yeye amuokoe?

9. Peter Keating anaendelea kumshawishi Howard Roark kwamba hilo ni jambo la kujitolea kwa kufanya hivyo atakuwa ametoa mchango wake kusaidia maskini wanaoishi kwenye mabanda wawe wamepata makazi ya bei rahisi kitu ambacho kitampa kuridhika kwa kufanya jambo bora namna hiyo. Howard Roark anamwambia hiyo kwake bado haiwezi kuwa sababu ya kumshawishi.

10. Peter Keating akaendelea kwa kumshawishi kwamba kwa kufanya hivyo atakuwa anafanya kile anachokipenda na kufurahia. Howard Roark akamwambia sasa ameanza kuongea lugha yake.

11. Howard Roark anamwambia Peter Keating kwamba ana uzoefu mkubwa sana kwenye miradi hiyo ya nyumba za watu wa kipato cha chini, chini hata zaidi ya kiasi kilichopendekezwa. Anamwambia hivyo atafanya kazi hiyo, sio kwa sababu anataka kusaidia maskini kwani yeye hayuko kwa ajili ya kusaidia yeyote bali kwa sababu anataka kuona mradi wa watu wa kipato cha chini ukitekelezwa.

12. Howard Roark anaweka masharti kwamba atafanya kazi hiyo kwa masharti kwamba jengo hilo ni lazima lijengwe kadiri ya michoro yake na kisibadilishwe au kuongezwa kitu chochote. Baada ya hapo yeye hatajali kingine chochote.

13. Anamwambia Peter Keating kwamba anaweza kuchukua hiyo pesa yote peke, aandike jina lake kwenye mradi huo na amiliki kila kitu lakini wasibadilishe chochote kutoka kwenye original design.

14. Howard Roark akatoa karatasi mfukoni na kumsainisha Peter Keating na yeye kusaini makubaliano hayo. Akasema hakuna mwanasheria katika makubaliano yao lakini ndio ushahidi wake kwamba hatakubali kuona kazi hiyo ikifanyika tofauti na makubaliano.

15. Peter Keating alipopeleka mapendekezo hayo kwa Ellsworth Toohey, alimsifia sana akamwambia ameweza kupatia vizuri mno na akamfurahia sana.

16. Urafiki kati ya Howard Roark na Gail Wynand umeimarika sana, wana ukaribu wa hali ya juu sana. Gail Wynand ameendelea kumletea Howard Roark miradi mingi sana ya ujenzi na wamekuwa wakitumia muda mwingi sana pamoja.

17. Howard Roark amekuwa akiandikwa sana kwenye gazeti la Gail Wynand la “The Banner” na mara nyingi makala hizo zinaandikwa na Gail Wynand mwenyewe.

18. Austen Heller anajaribu kumwonya Howard Roark kwamba urafiki wake na Gail Wynand umekuwa mkubwa sana mpaka unatilia mashaka. Akajaribu kumshawishi Howard Roark awe makini na Gail Wynand huenda ana malengo yake ya tofauti.

19. Peter Keating anakutana na Catherine Halsey baada ya kupotezana kwa miaka mingi sana. Wanaongea na Peter Keating anamwambia kwamba anatamani kumwomba msamaha lakini anashindwa. Anajaribu kumwambia Catherine aseme chochote juu ya yaliyotokea ili roho yake itulie kwa sababu anajisikia vibaya sana.

20. Catherine anamwambia kweli alijisikia vibaya sana, aliumia kiasi kwamba mjomba wake Ellsworth Toohey alimletea daktari. Anasema aliwahi hata kuzimia akiwa mjini. Anamwambia pia kwamba alifurahi kusikia kwamba ameachana na Dominique kwa sababu kama ameweza kuolewa na mtu kama Gail Wynand basi hakuwa mtu sahihi sana kwake.

21. Gail Wynand na Howard Roark wanaondoka na kwenda safari ya miezi mitatu. Huko wanakuwa na mengi sana ya kuzungumza hususan falsafa mbali na namna maisha yao yanavyohusiana nazo.

22. Peter Keating anakamilisha michoro na kuanza ujenzi wa mradi wa Cortlandt. Ellsworth Toohey anawaingiza Gordon L. Prescott na Gus Webb kama washirika wake. Peter Keating anawakataa na kusema atafanya kila kitu peke yake lakini Ellsworth Toohey anahimiza wawepo kwani wao pia wanahitaji kuimarika zaidi na Peter Keating anashindwa kuwazuia.

23. Gordon L. Prescott anaingiza mabadiliko na maboresho kwenye mradi huo na kubadili vipengele kadhaa. Pia kuna wanaongeza eneo la mazoezi ambalo halikuwepo kwenye kazi ya mwanzoni.

24. Peter Keating anajitahidi kupambana kusiwepo na mabadiliko lakini inamuwia vigumu. Gordon L. Prescott anasema inabidi na wao waweke mchango wao kwenye kazi hiyo kama washirika kwenye upande wa ushauri wa kitaalamu kwani wanaona kazi haijafanyika ipaswavyo.

25. Peter Keating anaenda kwa Howard Roark kumuuliza sasa atafanya nini kwa hayo yaliyotokea. Howard Roark ambaye naye alishaona mabadiliko hayo anamwambia hawezi kumlaumu kwa chochote kwani ni makosa yake mwenyewe.

26. Howard Roark anamwambia alishafanya makosa ya hivyo kwenye mradi wa Cosmo-Slotnick na hata chuoni Stanton hivyo ni yeye mwenyewe ni sehemu ya makosa hayo. Hivyo sasa anakwenda kufanya maamuzi magumu ambayo yatamletea wakati mgumu sana Peter Keating lakini yatamletea wakati mgumu zaidi yeye mwenyewe Howard Roark. Lakini hata hivyo hana budi kufanya hivyo.

Ahsanteni.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *