UBORA KWENYE UJENZI HAUNA MBADALA.

Ikiwa mtu ameniuliza ni kitu gani cha kwanza utamshauri mtu yeyote anayetaka kuanza ujenzi wa mradi wa jengo lake kuweka kipaumbele? Nitamjibu bila kusita wala kumung’unya maneno kwamba zingatia ubora katika kila hatua.

Suala la ubora katika mradi wa aina yoyote wa ujenzi ni jambo ambalo bado halipewi uzito unaostahili. Hiki ni kitu ambacho kinashangaza sana kwamba inakuwaje kitu muhimu kama ubora katika ujenzi kinashindwa kupewa kinapumbele namba moja na watu wote wanaohusika kwenye ujenzi?

Kwa haraka haraka ni rahisi mtu kufanya maamuzi ya kutafuta njia za mkato kuanzia gharama mpaka muda kwa kitu ambacho kinadumu miaka mingi kama nyumba au jengo bia kufikiria hasraa na gharama ambazo anaenda kuingia kwa kupitia njia za mkato.

Ukweli ni kwamba suala la gharama na muda linakuwa na uzito wakati wa utekelezaji peke yake lakini mara baada ya kumaliza suala la utekelezaji kitu chenye umuhimu na kitakachokupa furaha ya kudumu ni kama kazi husika imefanyika kwa viwango bora.

Ubora katika ujenzi unaanzia kuanzia wakati wa kutengeneza ramani ambayo inatakiwa kufanyika katika utaalamu wa hali ya juu kuanzia mpangilio wa kimatumizi mpaka mwonekano bora kabisa wan je. Kisha utekelezaji wa ujenzi wa mradi husika unapaswa kuwa unafuata taratibu zote na umakini na usahihi wa haki ya juu ili mwisho kile kilichokusudiwa kifanyika katika viwango bora kabisa.

Jambo la muhimu kabisa la kuzingatia ni kwamba suala la ubora halina mbadala wake, yaani kazi ni lazima iwe na ubora na hakuna namna nyingine ikiwa wahusika walioifanya wanahitaji kuridhika na kuepuka majuto ya baadaye kuanzia mara baada ya kazi hiyo kumalizika.

Hivyo ni muhimu sana mradi wowote wa ujenzi uanze kuweka kipaumbele kwenye ubora kabla ya jambo lolote lile kuanza kufanyika.

Ahsanteni.

Karibu kwa Maoni au Maswali.

Whatsapp/Call +255717452790.

Architect Sebastian Moshi.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *