UJENZI USIKUUMIZE KICHWA, OMBA USHAURI KWA WATAALAMU.

Mara nyingi makosa makubwa yanafanyika kwenye ujenzi yakiambatana na hasara kubwa kwa sababu tu ya mhusika mfanya maamuzi kukosa ushauri sahihi kwenye mradi wake. Kama tunavyojua kila eneo kwenye maisha lina utaalamu wake na kukosekana kwa utaalamu huo mara zote huambatana na makosa ambayo yangeondolewa au kupunguzwa kwa mtu kutafuta ushauri sahihi kwenye eneo husika. Na ushauri bora na sahihi unatokea kwa mtu aliye na ujuzi wa kitaalamu na uzoefu wa eneo husika.

Sasa huwa ni jambo la kushangaza pale ambapo unakuta mtu anahangaika na kuteseka na jambo asilokuwa na ujuzi wa kitaalamu nalo wala uzoefu nalo na mwisho anaishia kufanya maamuzi yasio sahihi na kuingia kwenye hasara na majuto wakati wataalamu husika wapo na wapo kwa ajili yake. Mtu unapojaribu kuumiza kichwa kuhusu ujenzi unapaswa kujua kwamba kuna watu hiyo ndio kazi yao wanayofanya kila siku kwa miaka mingi na ndio wanaoshughulika pia na mamlaka zote zinazodhibiti fani ya ujenzi hivyo wanafahamu mengi sana ambayo hufahamu.

Kwa kuwauliza watu hao utakuwa umetua mzigo mkubwa wa mawazo na ukiwa uko huru zaidi kwani umefahamu mambo muhimu sana unayokwenda kushughulika nayo. Usikubali kabisa kupata ushauri kwa watu wasio sahihi na wanaobahatisha mambo bali hakikisha umepata mtaalamu mbobezi katika eneo hilo ili ufanya maamuzi ya uhakika. Watu wote ambao hutafuta ushauri wa kitaalamu kabla ya kufanya ujenzi mwishoni hujikuta wakifurahia na kujivunia kazi zao huku wakiwa wamefanya kazi zao wakiwa wenye furaha na amani kubwa moyoni.

Tuwasiliane.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *