JENGA GHOROFA KWA GHARAMA KARIBU SAWA NA NYUMBA YA CHINI.

Watu wengi wamekuwa wakitamani sana kujenga ghorofa katika maisha yao. Hii ni kwa sababu katika hali ya kawaida inaaminika kwamba nyumba ya ghorofa ni ni ya hadhi ya juu kuliko nyumba ya chini isiyo ya ghorofa. Lakini kwa sababu thamani ya vitu kwenye jamii huwa vinatokana na vile inavyokubalika na wengi hivyo basi nyumba ya ghorofa ina hadhi ya kipekee ukilinganisha na nyumba ya kawaida isiyo ya ghorofa. Hivyo kwa kujenga nyumba ya ghorofa kwa usahihi mtu anakuwa ameionyesha jamii kwamba yeye ni mtu mwenye hadhi ya tofauti.

Lakini hata hivyo mtu unapoamua kujenga nyumba ya ghorofa maana yake unakuwa pia umeweza kuokoa sehemu ya eneo la ardhi yako ambayo ilikuwa inachukuliwa na vile vyumba ambavyo vimepanda juu badala ya kujengwa chini. Hivyo unakuwa umejenga nyumba kubwa zaidi lakini bila kutumia eneo kubwa sana la kiwanja chako ambacho aidha utafanyia mambo mengine au utakuwa na eneo kubwa ya bustani na maeneo ya kufanyia vitu vingine nyumbani kwako. Eneo hili la ardhi unalokuwa umeliokoa lingeweza kukugharimu pesa nyingi kulipata lakini umelipata kwa kujenga ghorofa.

Jambo lingine ni kwamba ukweli ni kwamba jengo la ghorofa likifanyika vizuri lina nafasi ya kuwa na mvuto kwa kiasi kikubwa sana ukilinganisha na nyuma ya chini isiyo ya ghorofa. Yaani jengo la ghorofa likipangiliwa vizuri lina nafasi ya kukuvutia kimwonekano na ukalipenda kuzidi jengo la kawaida lisilokuwa la ghorofa. Jengo la ghorofa pia lina nafasi ya kukupatia hewa safi na nyepesi zaidi kwa vile vyumba vya juu kuliko chini na hasa kama eneo lako liko kwenye mwinuko au karibu na eneo la wazi, ufukwe wa bahari, ziwa mto n.k., Hali kadhalika jengo la ghorofa litakupa kuona “view” inayopendeza macho yako.

Hata hivyo changamoto kubwa inayoongoza kuwafanya watu kukimbia na kuogopa kujenga ghorofa huwa iko kwenye gharama za ujenzi. Watu wengi wanaamini kwamba ujenzi wa nyumba ya ghorofa ni wa gharama sana kiasi kwamba hawataka hata kuifikiria kama moja kati mbadala wa aina ya ujenzi wake wa nyuma. Kiuhalisia ni ukweli kwamba ujenzi wa ghorofa ambayo eneo la ujenzi(built) area inalingana kwa kila kitu ni gharama zaidi ukilinganisha na nyumba ya chini isiyo ya ghorofa, lakini katika mazingira ambayo eneo la ujenzi linalingana kwa kila kitu utofauti wa gharama ni mdogo sana kwani ni ule mfumo wa mihimili pekee ndio unaoongezeka. Lakini pamoja na hayo bado faida za kujenga ghorofa kama tulivyoziona hapo juu ni nyingi sana kiasi kwamba hazina hiyo gharama kiasi inayoongezeka inakuwa ni kama imefidiwa.

Sehemu ambayo gharama itakuwa ni kwamba ukilinganisha nyumba ya chini na nyumba ya ghoroa ni kwenye eneo la michoro ya ramani za ujenzi kwani jengo lisilokuwa la ghorofa linahitaji michoro ya usanifu peke yake wakati jengo la ghorofa linahitaji michoro ya usanifu sambamba na uhandisi, kwa maana hiyo gharama ya michoro ya ramani inakuwa kubwa. Lakini hata hivyo gharama za michoro ya ramani unapolinganisha na gharama za ujenzi bado ni gharama ndogo sana ukilinganisha na kile ambacho mtu anakwenda kukipata na ukilinganisha pia na gharama ambazo mtu anakwenda kutumia kwenye kununua vifaa vya ujenzi.

Hivyo basi ikiwa mtu unatamani kujenga nyumba ya ghorofa lakini una hofu juu ya mambo mbalimbali nakuhimiza usiwe na wasiwasi wala kuogopa bali nenda mbele na timiza ndoto yako hiyo kwani unachoenda kufanya ni maamuzi sahihi ambayo sio rahisi uyajutie.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *