RAMANI YA NYUMBA YAKO.

Imekuwa kawaida sasa kwa baadhi ya watu kutokana na kutokujua undani wa kazi za ramani za ujenzi wamekuwa wakipenda kazi fulani na kutaka kujua kama kazi hiyo inaweza kufanyika kama ilivyo, na ajabu zaidi ni kutaka ifanyike kama ilivyo. Kiuhalisia hakuna kazi rahisi katika design kama ambayo imeshapendekezwa, ninaposema rahisi simaanishi kwamba ni kazi ndogo kufanya Hapana, kazi kubwa iko pale pale lakini ukiwa unajua unapotakiwa kufika safari inakuwa nafuu kuliko kwenda ukiwa huna njia ya moja kwa moja ya kufika.

Nataka kumaanisha kwamba mteja hatakiwi kuwa na hofu kwamba kazi hii itashindwa kufanywa na huyu mtaalamu bali anachopaswa kuhofu ni kama kazi inayofanywa itatimiza mahitaji yake katika uhalisia, nikimaanisha mahitaji ya ndani kwa sababu watu wengi huvutiwa na kile wanachokiona kwa nje. Mtaalamu anaweza kufanya kwa kujaribu kulazimisha upate kile unachotaka kama ulivyoona na ukafanikiwa kupata kama kilivyo lakini baadhi ya mahitaji yakawa hayaendani na wewe au huyahitaji kabisa isipokuwa tu kwamba ulipenda muonekano.

Sasa je ni nini cha kufanya ikiwa unahitaji au utapenda nyumba yako ipendeze kama ile uliyoiona lakini hapo hapo iwe inaendana na mahitaji yako wewe na sio haya yaliyopo kwenye nyumba uliyoipenda. Kwanza kabisa unapaswa kuamini kwamba unaweza kufanyiwa nyumba yako nzuri saw ana ile uliyoipenda au hata zaidi bila kuiga ile moja kwa moja. Pili ni kumwonyesha mtaalamu nyumba hiyo uliyoipenda na kumwambia kwamba unahitaji nyumba hiyo iwe na sifa na mpangilio unaofanana na hiyo uliyoipenda lakini mahitaji yako yawe yale unayotaka wewe. Hapo mtaalamu atakachofanya ni kujumuisha vipengele na mipangilio ya kisanifu inayofanana na ile uliyoipendekeza lakini bila kulazimisha mahitaji ya ndani kuendana na ile nyumba nyingine.

Mwisho wa siku utapata nyumba yako nzuri inayoendana na mahitaji yako lakini iliyojumuisha mipangilio kama iliyokupendeza kwenye lile jengo lingine na kuchanganya na mingine ya mtaalamu na hivyo kuwa na nyumba yenye kuvutia kuzidi hata hiyo nyingine. Muhimu ni mtaalamu husika au na uwezo mkubwa katika fani ya usanifu majengo au ambaye ana timu yenye uwezo mkubwa katika fani ya usanifu majengo na ujenzi na utafanikisha kupata kazi nzuri sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *