MRADI WA UJENZI UKIKOSA USIMAMIZI SAHIHI LAZIMA KUNA KITU KITAHARIBIKA.

Katika maisha hakuna kitu kigumu kama kutabiri mambo yatakayotokea kwenye jambo lolote ambayo hayaonekani katika hali ya kawaida. Mara nyingi mtu anapowaza jambo lolote ambalo linahusisha mchakato fulani kwenye utekelezaji wake huwa anawaza kwa kudhania kwamba kila kitu kitafanyika kwa usahihi na uhakika bila hata kujali uwezo, umakini na mwongozo walionao watendaji wa mradi husika. Hii ni licha ya kwamba watu wanaweza kuwa aidha hawana uhakika au wanajua kwamba watendaji wa mradi husika kuna utaalamu fulani wanaukosa.

Sasa kinachokuja kutokea hutegemea na kama watendaji husika wamefikia uwezo, wana umakini sahihi au kuna mwongozo fulani wanaoufuata katika utekelezaji wa mradi husika wa ujenzi. Inapotokea kwamba mradi wa ujenzi unafanyika bila kuwepo mhusika mwenye utaalamu uliowekwa katika mradi huo au kukosekana kwa mwongozo wa mchakato unaofuatwa ili kuhakikisha kwamba hakuna hatua inayorukwa katika utekelezaji wa mradi husika, kuna matatizo hutokea kutokana na maamuzi ya baadhi ya mambo kufanywa na mtu asiye na taaluma husika kwa sababu pia mwongozo sahihi wa mchakato mzima kukosekana.

Hivyo mradi wowote wa ujenzi unaofanyika ni aidha inabidi kuwepo kwa wataalamu husika ambao watatoa maamuzi sahihi katika maeneo husika yanayohitajika au kuwepo kwa mwongozo wa mchakato mzima wa utekelezaji wa mradi ambapo kila kinachofanyika kinakuwa kimeshajibiwa kwenye mchakato na ikiwa limetokea jambo ambalo halipo katika orodha ya mchakato basi maamuzi hayatafanywa na kila mtu bali mpaka mtaalamu husika afike au atoe ufafanuzi au maamuzi kwa njia nyingine. Kwa namna hii tutaweza kuepuka changamoto nyingi zinazotokana na kukosekana kwa maamuzi sahihi katika miradi ya ujenzi na wakati kuhusisha hasara kubwa.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *