KUTUMIA MFUMO KWENYE MRADI WA UJENZI KUNAPUNGUZA UTEGEMEZI WA MTU.

Katika miradi yetu ya ujenzi kwa mazoea ya kawaida mara nyingi huwa kuna mtu ambaye ni mwenye uwezo mkubwa na mzoefu ambaye ndio huwa tunamtegemea yeye katika maamuzi mengi muhimu na anapokosekana watu wengi wanakosa imani na kazi inayoendelea. Jambo hili limekuwa linasababisha hata baadhi ya wateja kupata mashaka na wakati mwingine kupoteza imani ya kutoa kazi husika kwa kuhofia ikiwa mtu fulani hayupo basi kazi hiyo inaweza kuharibika au kupata hitilafu nyingine yoyote. Kwa kifupi uwepo wa mtu huyo ndipo imani ilipojengeka.

Hata hivyo utegemezi wa kiwango cha juu namna hiyo kinakuja na changamoto nyingi, kwanza mtu huyo anapobanwa na kazi nyingi au majukumu mengine yoyote au kushindwa kupatikana kwa sababu nyingine yoyote kazi husika huweza kusimama na kusababisha upotezaji mkubwa wa muda. Lakini pia mtu yeyote anapokuwa ni tegemeo sana basi huweza kuwa tatizo kwani anaweza kuyumbisha watu na kazi yenyewe na kupelekea matatizo makubwa ikiwemo kusababisha uharibifu. Mwisho mtu huyo anaweza kufikia sehemu akawa hashauriki hata kama anakosea na kwa sababu anaamini na kuhusudiwa sana basi inakuwa kazi ngumu kumlazimisha kubadilika na hivyo kuleta matatizo makubwa.

Suluhisho la changamoto hii ambayo imekuwa ikipatikana sana maeneo mengi ni kutumia mfumo ambapo kila mtu anakuwa sehemu tu ya mfumo na sio kutegemewa. Kwa kutumia mfumo kila kitu kimeshapangiliwa na maeneo yanahitaji maamuzi mazito tayari zimeshapingiliwa namna ya kufanya na haihitaji mtu mwenye uwezo wa juu kabisa kuufanya. Kwa sababu kinachofuatwa ni mfumo basi mtu yeyote anaweza kusimamia utendaji wake. Kwa kifupi katika mfumo mambo hayafanyiki tena kutoka kwenye kichwa cha mtu bali karibu kila kitu kinajulikana na wafanyakazi wote husika wa kitengo cha ujenzi na ukandarasi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *