MIKOPO YA UJENZI WA NYUMBA (MORTGAGE) INAPATIKANA TANZANIA.

Ni jambo ambalo liko wazi kwamba inapokuja suala la ujenzi wa makazi kibiashara kwa nyumba za biashara na nyumba za kuishi za watu binafsi kwa mikopo ya nyumba ya masharti ya kukabidhi hatimiki (mortgage) kwa Tanzania bado ni eneo lenye changamoto na ambalo bado halijaimarika sana pia. Hii ndio maana kwa watu wengi hata neno lenyewe. “mortgage” ni msamiati mgeni sana kwenye masikio yao. Watu wengine wengi pia walishakata tamaa kwenye eneo hili na hivyo watu wengi wanachukua mikopo kwa namna nyingine au hata kutafuta fedha zao wenyewe ili kujenga zao na nyumba za ndoto zao.

Hata hivyo, habari njema ni kwamba hapa Tanzania tayari kuna taasisi kadhaa zinatoa mikopo ya aina hii ya “mortgage” yenye viwango mbalimbali vya riba pamoja na vigezo na masharti mengine. Licha ya kwamba bado ni eneo lisilo na umaarufu mkubwa lakini eneo hilo linaendelea kukua na taasisi hizi zinatofautiana vigezo na masharti ya kupata mikopo hii. Mikopo hii ya nyumba “mortgage” imekuwa inarahisishia sana watu mzigo mkubwa wa ujenzi wa nyumba za kuishi hususan vijana wanandoa ambao wanahitaji kuanza maisha mapya ya ndoa katika mazingira mazuri na tulivu ya kulea watoto na kujenga familia zao katika maadili sahihi.

Mikopo hii ya mortgage imegawanyika kulingana na taasisi, ya kwamba kuna taasisi ambazo zinatoa mkopo wa kujenga nyumba yote kuanzia mwanzo mpaka mwisho kupitia kulipa wakandarasi na wasambazaji wa vifaa moja kwa moja. Kuna taasisi nyingine zinatoa mkopo ikiwa mradi husika wa ujenzi umefikia hatua fulani ya mbele baada ya kuvuka hatua ya mwanzoni kisha mkopo huo kumalizia ujenzi wa nyumba husika. Taasisi nyingine zinatoa kiwango fulani cha mkopo kisha mteja anamalizia kiwango kilichobakia kwa mfano taasisi ya kifedha inaweza kutoa mkopo kwa 80% kisha kumtaka mteja kumalizia 20% iliyobakia.

Karibu sana tuwasiliane.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *