MRADI WA UJENZI UNAHITAJI MAANDALIZI MAKINI SANA KABLA ILI KUEPUKA USUMBUFU BAADAYE.

Ni wazi kwamba kwa mtu yeyote ambaye amewahi kujenga na kusimamia ujenzi wake mwenyewe anajua ni jinsi gani mradi wa ujenzi unavyoambatana na changamoto na usumbufu mkubwa wakati wa utekelezaji wake hasa kama hakukuwa na maandilizi na mikakati madhubuti mwanzaoni. Katika usumbufu huu kitu ambacho hugharimu sana ni muda ambao mradi huo unachukua katika kufuatilia mambo mbalimbali na usumbufu ambao unaweza kupoteza zaidi muda na kuchosha ni ikiwa mamlaka husika nazo zitaanza kuufuatilia kama umekidhi vigezo vyake na kupatiwa kibali cha ujenzi.

Kuepuka usumbufu na upotezaji mkubwa sana wa muda unaopelekea pia ujenzi kujengwa kwa viwango duni au kuwa wa hovyo kwanza mtu unapaswa kuanza kwa kutengeneza ramani bora sana ya ujenzi ambayo itakuvutia kiasi cha kukuhamasisha kuihangaika ukiona kabisa kwamba gharama unazoingia huzijutii kwani unaenda kupata kilicho bora sana. Pili ni kuhakikisha kwamba unafuatilia taratibu zilizowekwa na mamlaka husika mapema ili kukamilisha yote yanayohitajika na kukabidhiwa kibali cha ujenzi uweze kuepuka usumbufu, vitisho na adhabu zilizowekwa na mamlaka hizo ambazo zitakuumiza na hata kukukasirisha.

Kisha unapaswa kuhangaika sana kupata watu wa kufanya kazi hiyo ambao ni waaminifu sana katika kila eneo na wenye uwezo mkubwa wa kutosha kufanya kazi yenye viwango bora sana ili fedha yako nyingi sana unayokwenda kuitumia kwenye kujenga uwe umeitendea haki. Baada yah apo utahitaji kupata msimamizi mtaalamu mwenye kufahamu kanun izote sahihi za ujenzi na umuhimu wa kuhakikisha michoro imefuatwa na kama kutakuwa na mabadiliko yafanyike kwa namna ambayo hayavuruga au kwenda kinyume na kanuni za kitaalamu ambazo ndio zinazoamua ubora katika ujenzi. Mtaalamu huyo anaweza pia kuwa ndiye mjenzi mkuu ikiwa mtaridhiana na kukubaliana kwa masharti kutoka pande zote mbili.

Ukishakamilisha hatua hizo hatua nyingine muhimu iliyobakia ni kuhakikisha vifaa vya ujenzi vinapatikana kwa wakati na kwa usahihi ili kazi iende kwa muda uliopangwa kuepusha gharama kuwa kubwa zaidi kutokana na kucheleweshwa kwa kazi. Ikiwa vifaa unanunua wewe basi inabidi maandilizi ya vifaa husika yafanyike angalau wiki mbili kabla na hapo hapo vijulikane vinapatikana wapi na muda gani ili kuhakikisha pia kwamba kwenye hifadhi au duka vinakopatikana vinaweza kupatikana kwa wakati huo. Lakini kama mjenzi mwenyewe ndiye amechukua mradi huo mpaka kukamilika basi hilo jukumu litakuwa ni la kwake na anapaswa kuhakikisha anafuata mpango kazi aliokupa kukamilisha kazi hiyo. Kwa maandilizi hayo kwa upande wako utaepuka kwa kiasi kikubwa usumbufu na kupoteza muda mwingi kunaletwa na mradi wako wa ujenzi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *