GHARAMA ZA UJENZI NI MAKADIRIO TU HUWEZI KUJUA KWA UHAKIKA KABLA YA KUJUA UKUBWA HALISI.

Kila siku tunawasiliana na watu wengi ambao wanapiga simu au kutuma ujumbe kwa njia ya whatsapp na kawaida wakiulizia mambo mbalimbali yanayohusu ujenzi. Moja kati ya vitu vinavyouliziwa sana na kwa namna tofauti tofauti ni gharama za ujenzi. Watu mbalimbali wanaulizia gharama za ujenzi wa majengo ya aina mbalimbali na ya ukubwa mbalimbali kwa kutaja wakiamini kwamba wanaweza kupewa jibu moja la kuhusu gharama hizo mara moja na kwa uhakika.

Lakini katika uhalisia hilo sio jambo linalowezekana kwa sababu kwanza hata kwa miradi ya kawaida ya serikali na taasisi nyingine gharama za ujenzi licha ya makadirio yanayofanywa na wataalamu husika waliobobea sana kwenye taaluma ya ukadiriaji majenzi bado huwa vigumu kupata gharama halisi. Lakini pia kwa mradi unaouliziwa bado sio utakaojengwa au angalau mazingira ya ujengaji wake hayatafanana, na hata hivyo bado ni vigumu sana kwa mradi husika kujengwa kama ulivyopendekezwa.

Hivyo mtu unapoulizia gharama za ujenzi kisha ukajulisha ni kiasi fulani, bado katika uhalisia sio rahisi iwe ni kiasi hicho kama ulivyoelezwa bali hata yatakuwa ni makadirio ambaye kutegemea na namna mhusika alivyokuelewa yanaweza kuwa mbali kabisa na uhalisia. Lakini kama utaeleza vizuri na kueleweka kwa usahihi basi kuna uwezekano wa kupatiwa makadirio yanayokaribiana na uhalisia.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *