MRADI WA UJENZI UWEKEWE VIWANGO KABLA YA KAZI KUANZA.

Licha ya kwamba siku hizi kumekuwa na na maendeleo makubwa ya kiteknolojia na kitaaluma ambayo yamepelekea kufanyika kwa kazi za michoro zinazoonyesha kila kitu kinachokwenda kufanyika kitakavyokuwa kabla hata ya ujenzi kuanza lakini bado kumekuwa na changamoto ya wahusika kufikia viwango ambavyo vinatarajiwa kwenye kazi za ujenzi. Jambo hili limekuwa likichangiwa na kutokuwepo kwa makubalianao yoyote ya viwango na namna kazi husika inakwenda kufanyika na kufanikiwa katika matokeo ya mwisho. Katika uhalisia ni kwamba licha ya uwepo wa michoro na maelekezo yote bado sio kila kitu kinaweza kuelezewa kupitia michoro bila kuwepo kwa makubaliano mengine nje ya kile ambacho michoro na picha zake vinaonyesha.

Kwa sababu ya mazoea na kukosekana kwa vikao vya wataalamu kujadili maendeleo ya kazi ya uejnzi inayoendelea, watu wamekuwa wakifanya kazi vile wanavyojiamulia na kufikiri bila kuwepo kwa muongozo uliamuliwa na wataalamu pamoja na mteja, jambo linalopelekea matokeo ya mwisho wakati mwingine kutokuwa yale yaliyokusudiwa. Kuna watu wengi sana wanaweza kuhusika na kila mtu kupanga lake vile anavyofikiri na hata kutoa ushauri bila kuzingatia kanuni zozote na ukatekelezwa na kuja na aina nyingine ya matokeo ambayo inaweza kuwa haijaridhia na wadau husika wa mradi. Jambo hili limetokea mara nyingi na katika miradi tofauti ya ujenzi na kusababisha hata kukosekana kwa kile kilichotamaniwa.

Hivyo ni muhimu kuwe na vikao muhimu vya mwanzoni ambavyo vitajadili kuhusu matokeo yanayokusudiwa na namna yanakwenda kupatikana kupitia namna ya utekelezaji. Matokeo yanayotazamiwa yatapaswa kupangwa na timu ya wataalamu kwa ushirikiano wa karibu sana na mteja husika wa mradi au wawakilishi wake sahihi. Matokeo yanayotazamiwa yatasababisha hata mabadiliko katika utekelezaji wa mradi katika maeneo kadhaa kuanzia vifaa vinavyokwenda kutumika, aina ya watu na utaalamu unaokwenda kutumika katika mradi husika. Matokeo hayo tarajiwa yatapaswa kuandikwa katika maandishi ambayo ndio yatatumika sambamba na mwongozo wa utekelezaji na kusimamiwa na wataalamu ambao ndio watakaohakikisha mchakato unaoendelea unaelekea kwenye matokeo yanayotazamiwa.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *