UJENZI WA TOFALI ZA KUCHOMA DAR ES SALAAM.

Tofali za kuchoma zimekuwa zikitumika zaidi na kukubalika maeneo mbalimbali duniani. Hata hivyo kwa Tanzania zimekuwa zikitumika zaidi yale maeneo au mikoa ambapo zinapatikana kwa urahisi. Lakini watu mbalimbali, kwa sababu mbalimbali wamekuwa wakizipenda na kutamani kuzitumia sio tu kwenye maeneo zinakopaatikana kwa urahisi bali hata kwenye mikoa na miji ambapo hazipatikani kiurahisi. Jambo hili limekuwa likisababisha usumbufu kwa watu wa maeneo ambapo tofali hizi hazipatikani na zinahitajika kwa matumizi.

Dar es Salaam ni moja ya maeneo ambapo tofali za kuchoma ni hadimu sana kupatikana licha ya kuwepo kwa uhitaji wa tofali hizo. Dar es Salaam na sehemu kubwa ya ukanda wa pwani kuna ardhi yenye udongo wa mchanga zaidi ambao sio sahihi sana kwa kutengenezea tofali za kuchoma na hivyo tofali zinazopatikana kwa wingi na kwa urahisi ni tofali za mchanga na saruji. Hata hivyo kwa wahitaji wa tofali za kuchoma waliopo Dar es Salaam tofali hizi zinaweza kupatikana kwa karibu zaidi kutokea Morogoro Kingolwira umbali wa kilomita zaidi ya 150 kutokea Dar es Salaam.

Hivyo ikiwa mtu anahitaji tofali hizi kwa Dar es Salaam ni vyema kuzichukua kwa wingi kwa kuagiza mzigo mkubwa kutoka Morogoro, Kingolwira. Vinginevyo ikiwa mtu unahitaji urembo wa kuchorea katika tofali bado hata tofali za mchanga na saruji zinaweza kuchorewa na kupendeza sana na baadhi ya watu wenye kupenda umaridadi huo wamefanya hivyo.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *