PICHA ZA MUONEKANO WA JENGO ZINATOA MWONGOZO MUHIMU KWA WAJENZI.
Baadhi ya watu wamekuwa wakiona kwamba kufanya kazi ya michoro ni gharama sana na hivyo wamekuwa wakijaribu kutafuta njia za mkato za gharama nafuu katika kuvuka hatua hiyo. Katika kufanya hivyo watu hao wamekuwa wakiruka baadhi ya hatua za kazi ya usanifu na hasa hatua ya kutenegenza muonekano wa jengo kwa ubora ili kupunnguza kazi hiyo ya michoro waweze kupata urahisi na unafuu kwenye gharama. Hii ni kwa sababu wanaamini hatua hiyo haina umuhimu mkubwa kwani mwishoni wanaweza tu kufika mwisho kwa mwongozo wa ile ramani ya sakafu ya chini.
Ukweli ni kwamba watu hao wanahujumu kazi zao wenyewe bila hata wao kujua kwa sababu kwanza kwa kukwepa hatua hiyo ya muonekano wa jengo unakuwa unaweka ugumu mkubwa kwenye michoro mingine mingi muhimu ambayo inahitajika kutoa mwongozo uliokamilika kwa kazi husika ya ujenzi. Michoro hiyo ni ramani ya mbele na nyuma, upande wa kulia na kushoto, ramani ya sehemu ya ndani iliyokatwa inayoomyesha taarifa za msingi na pamoja na ramani ya paa ambazo zote zinarahisha na mchoro wa muonekano mzima wa jengo katika picha.
Lakini pia muonekano bora wa jengo katika picha ni muhimu sana katika kutoa mwongozo sahihi wa kule kazi hiyo inakoelekea na hivyo kuepusha hatari ya kufikisha mbali ujenzi ukiwa na makosa. Muonekano wa nje utaonyesha haraka sana makosa hayo kabla kazi hiyo haijafika mbali na hivyo hatua sahihi kuchukuliwa mapema kuepusha hasara na uharibifu.
Karibu sana.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255 717 452 790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!