ANZA MRADI WAKO WA UJENZI UTAMALIZA.

Kutoka kwenye uzoefu wa watu wengi sana niliokutana nao mara nyingi watu huanza miradi yao ya ujenzi wakiwa hawana uhakika kama wanakwenda kukamilisha miradi hiyo na huanza kama utani tu wakiwa hawajui ni lini watakamilisha miradi yao. Lakini kwa sababu baada ya mtu kuanza huweka nguvu na akili zake zote kwenye mradi huo wa ujenzi hujakuta anapeleka pesa nyingi sana kwenye ujenzi ambazo pengine angepeleka katika mambo mengine ambayo yanaweza kuwa pia sio muhimu sana. Kwa kuweka nguvu kubwa na na kuweka bidii sana kwenye kutafuta namna ya kukamilisha mradi huo hujikuta akipiga hatua kubwa za haraka zaidi kuliko alivyotegemea.

Kisha baada ya kupaua na kuweka milango na madirisha wakati akiwa hajafanya kitu chochote cha ziada wengi huamua kuhamia katika nyumba hiyo baada ya kumalizia chumba kimoja au viwili na hapo ndipo huanza safari ya kumalizia taratibu. Kwa kuwa mtu anaishi kwenye nyumba hiyo hiyo na anatamani sana kuona imemalizika ili impunguzie kero na kumuongezea hadhi kwenye jamii huongeza kasi ya kuimalizia taratibu huku akijibana kwenye mambo mengine mpaka anakuwa amekamilisha kila kitu ndani ya nyumba yake.

Hivyo ikiwa mtu unapata wasiwasi wa kuanza ujenzi kwa kuhofu kwamba labda hutamaliza au itakuwa ni kazi ngumu kwake napenda kukutia moyo kwamba anza hiyo safari sasa na akili yake itaweza kupeleka kipaumbele huko na utapata fursa nyingi za kumalizia ikiwa umedhamiria kweli. Watu wengi nimekutana nao katika tasnia hii ya ujenzi ambao hawakutegemea kwenda kasi namna hiyo wengine wamekamilisha ndani ya muda mfupi kuliko walivyotegemea na wengine wamepiga hatua nzuri sana.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *