TABIRI MRADI WAKO WA UJENZI KWA KUTUMIA MFUMO.
Miradi ya ujenzi hasa miradi midogo na ya saizi ya kati imekuwa ni miradi isiyoisha changamoto katika mchakato wa ujenzi wake kwa sababu ya utata mwingi uliopo katika mfumo mzima wa uendeshaji. Utata wa miradi ya ujenzi inaanzia kuanzia kwenye uaminifu, uwezo, uzoefu na uzingatiaji wa taaluma husika za ujenzi katika vitengo husika. Mjumuisho wa changamoto hizo ndio zimekuwa chanzo cha kuzalisha matatizo yasiyoisha katika miradi ya ujenzi miaka nenda rudi. Lakini suluhisho kwa sehemu kubwa ya changamoto hizi lipo nalo ni kuendesha mradi kwa mfumo imara unaoendeshwa na watu.
Mfumo madhubuti wa uendeshaji wa miradi ya ujenzi unapatikana kwa kuleta pamoja mjumuiko wa mambo mengi kuanzia kanuni za kitaaluma, uendeshaji na usimamizi, uzoefu na uhusiano sahihi na wateja. Mfumo wa uendeshaji unaendelea kukua kupitia makosa madogo madogo ya kila siku ambapo mfumo unaendelea kuboreshwa kupitia suluhisho la makosa hayo ambayo mengine ni madogo sana kiasi kwamba tunaweza kusema ni uzembe tu na sio changamoto halisi lakini kupitia mfumo madhubuti wa uendeshaji basi huo uzembe mdogo mdogo unakomeshwa kabisa.
Hata hivyo faida za kutumia mfumo hazipo tu kwenye usahihi na uhakika wa kukamilisha mradi katika viwango bora na ndani ya muda bali mfumo madhubuti wa uendeshaji unasaidia pia mteja na wadau mbalimbali kuweza kutabiri ubora, muda na gharama za mradi husika. Hili linawezekana kupitia mfumo kwa sababu kwanza mfumo unajivunia uzoefu ambao unahusika katika maeneo yote ya uendeshaji wa mradi wa ujenzi kuanzia utendaji, muda, gharama na uwezekano wa kutokea kwa changamoto wakati wa utekelezaji. Uwezo huu wa kutabiri uelekeo wa kazi ya mradi wa ujenzi kupitia mfumo wa uendeshaji una msaada mkubwa mwanzoni mwa mradi au kabla ya mradi kuanza kufanya maamuzi thabiti ambayo yatapelekea mradi kukamilika kwa muda, kwa uhakika, kwa bajeti na kwa viwango sahihi vilivyoamuliwa.
Karibu sana kwa maswali, ushauri na kazi.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255 717 452 790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!