KUFIKA SITE NI MUHIMU KABLA YA KUFANYA HESABU YA GHARAMA ZA UFUNDI.

Mara zote huwa kuna utofauti unaotokea kati ya michoro ya jengo ikiwa bado haijajengwa na uhalisia wa jengo baada ya kuwa limejengwa. Utofauti huu huwa unakuwa na madhara kwa jengo husika ikiwa gharama za ufundi au ukarabati wake zitafanyika kwa kutegemea michoro peke yake bila mtaalamu wa gharama kufika eneo la ujenzo. Kiuhalisia gharama za ufundi hutegemea sana jengo lenyewe limejengwaje kuanzia ubora wa ufundi wenyewe mpaka mpangilio wa vipengele vya jengo ndani yake na namna vimefanyika ambayo sio rahisi kuelezewa kwa maneno au kuifikiria kwa kuangalia michoro.

Lakini pia ukiachana na uwezekano wa michoro kutofautwa kwa maana ya kupunguzwa au kuongezwa bado huwa kuna uwezekano wa kazi kufanyika kwa viwango duni kiasi kwamba kazi inayopaswa kufanyika juu yake inakuwa kubwa na ngumu zaidi kuliko inavyoweza kudhaniwa na kukubalika. Hivyo mafundi wengi hukutana na wakati mgumu sana wanapokuwa wamekubali kupatana kazi bila kuiona site na kisha baadaye wanapogundua kwamba kazi ni kubwa kuliko walivyodhani kupitia michoro wanajikuta wamejitwisha mzigo mzito sana ambao hawakuweza kuona hilo mwanzo.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *