PUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI KWA KIASI UNACHOTAKA MWENYEWE.

Hili suala la kupunguza gharama za ujenzi kwenye miradi ya aina zote za ujenzi limekuwa ni moja kati ya mijadala ambayo imekuwa ikijadiliwa wakati wote, tafiti nyingi zimefanyika na zinaendelea kufanyika kuja na mbinu zaidi za kuweza kupunguza gharama hizo. Ukweli ni kwamba gharama za ujenzi kwa mtazamo wa watu wengi kwa ngazi zote za miradi ni kubwa na zinahusisha michakato mbalimbali tata kuweza kufanikisha ujenzi bora na makini uliozingatia hatua zote muhimu za kitaalamu. Lakini watu wengi wanaotaka kupunguza gharama hizo ndio wamekuwa na mtazamo usio sahihi juu ya upunguzaji wake na wengine wamekuwa wakiamini katika miujiza badala ya kufikiri katika uhalisia.

Hata hivyo uhalisia wa gharama za ujenzi upo zaidi katika ukubwa na wingi kuliko katika vitu visivyoonekana au kuelezeka. Changamoto hujitokeza pale ambapo watu hutaka gharama za ujenzi zipungue bila kujua ni eneo gani haswa linalopunguzwa gharama hizo. Sasa sehemu kuu mbili ambazo zinazoweza kutumika kupunguza gharama za ujenzi ni moja kwenye ukubwa wa jengo lenyewe linalojengwa na mbili ni kwenye aina za vifaa vya ujenzi vinavyokwenda kutumika. Hivyo upunguzaji wa gharama za ujenzi ni kitu kitakachohitaji mjadala zaidi kati ya mteja na mtaalamu/wataalamu wa ujenzi. Mjadala huu utalenga zaidi kujadili umuhimu na madhara ya kuweka matumizi fulani na kutumia aina fulani za vifaa na madhara yake ambapo mwishoni kutakuwa na hitimisho zuri sana litakaloleta kuridhika kwa kila upande na hatua sahihi kuchukuliwa.

Mjadala huu utafanyika wakati kazi ipo katika hatua ya kuandaa michoro ya ramani na baada ya hapo katika hatua nyingine baada ya kukamilisha hesabu ya gharama za mradi husika. Mjadala wa michoro unafanyika wakati wa kuandaa michoro ya ramani ili kuhakikisha kwamba kila ukubwa unaoongezwa unakuwa na maana na umuhimu katika matumizi ya jengo hilo na kama hakuna umuhimu huo basi moja kwa moja inaondolewa. Mjadala mwingine utafanyika baada ya zoezi la kutengeneza hesabu ya gharama za ujenzi kukamilika. Hesabu hii itafanyika kuhakikisha vifaa vyote vinavyotumika vimejadiliwa na kuamuliwa kwa usahihi kwa kuzingatia gharama halisi na jinsi vinavyokwenda kuwa na madhara katika ujenzi huo sambamba na faida na na hasara zake.

Baada ya hapo mtu unakuwa umepunguza gharama za ujenzi kwa kiwango kikubwa sana kutokea kwenye gharama za awali ambazo hazikuwa zimezingatia umuhimu wa ukubwa na vifaa sahihi vya kutumika. Yote haya yanafanyika kwa kuhusisha wataalamu ambao gharama zao za kitaalamu ni ndogo sana ukilinganisha ni kile ambacho wanakwenda kukiokoa. Sasa ili kukamilisha zoezi lote hili kwa kutumia wataalamu wote kwa pamoja na kujadili nao yote haya kwa pamoja piga simu sasa tuwasiliane kwa namba za simu zilizopo hapa chini.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *