VIGAE/TILES ZINAZOTENGENEZWA KWA KUTUMIA ZEGE/CONCRETE TILES

Hizi ni aina ya vigae/tiles ambazo zinatengenezwa kwa kutumia zege yaani mchanganyiko wa mchanga na saruji, tofauti na hizi maarufu za sasa za ceramic na porcelain ambazo zinatengenezwa na mchanganyiko wa udongo wa clay, earthen, mchanga na malighafi nyingine. Hizi ni aina ya vigae/tiles zilizoanza kutengenezwa karne ya 18 na zimeendeelea kuwa maarufu sana mpaka katikati ya karne ya 20.

VIGAE/TILES ZA ZEGE

FAIDA ZA VIGAE/TILES ZA ZEGE

-Ni imara sana

-Zinadumu muda mrefu sana. Vigae/tiles za saruji zinadumu zaidi ya karne kadhaa na ni imara kuliko hata mbaona tiles za ceramic. Hili linazifanya ziweze kutumika sana maeneo yanayokanyagwa sana na watu wengi pia.

-Ni rahisi kusafishwa na kurekebishwa. Vigae/tiles hizi za zege zinaweza kusafishwa kwa kutumia dekio la mop linalonyonya maji vizuri na kuzifanya kurudia upya wake kila mara.

-Zimetengenezwa kutumika kwenye majengo ya aina zote za makazi na kwenye kila chumba bila kujali ni sebuleni, chumbani au kibarazani.

-Ni rafiki wa mazingira. Vigae/tiles za zege zinatengenezwa kwa kutumia malighafi za asili hivyo hazitegemei kuharibu mazingira ili kupata malighafi za kuzitengeneza.

-Licha ya kwamba huwa zinapata sana baridi nyakati za masika lakini zinaweza pia kupashwa joto nyakati hizi na baridi kali.

CHANGAMOTO ZA VIGAE/TILES ZA ZEGE

-Ni nzito sana na zinahitaji jengo liwe na mfumo wa mihimili ambao ni imara vya kutosha kubeba mzigo wote wa vigae/tiles hizi ambazo ni nzito sana. Hivyo zinahitaji mhandisi mihimili kufanya ukaguzi ili kujua kama mfumo wa mihimili una nguvu vya kutosha kubeba mzigo husika.

-Vigae/tiles hizi za zege ni nene kuliko vigae/tiles za kawaida hivyo unatakiwa kujua huenda zikapunguza kidogo kimo cha chumba zikaleta mpangilio usiotarajiwa.

-Kwa kawaida zege hupitisha maji hivyo zinaweza kunyonya na kushikilia maji na kuleta usumbufu wakati wa kufanya marekebisho au kuzibadili.

-Kwa kawaida vigae/tiles za zege huwa zina baridi sana.

VIGAE/TILES ZA ZEGE

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call 255717452790

Kupata makala bora za ujenzi tembelea website yetu www.ujenzimakini.com

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *