VIGAE/TILES ZINAZOTENGENEZWA KWA UDONGO NA MCHANGA.

Ukiachana na vigae/tiles zinazotokana na aina tofauti tofauti za mawe na miamba zinazochimbwa kama madini na kuchongwa katika saizi tofauti tofauti kutengeneza vigae/tiles, vigae vingi vinavyotumika katika majengo vinatengenezwa katika mashine kwa mchanganyiko wa udongo wa aina tofauti tofauti na mchanga kisha kupakwa rangi na kuwekewa urembo kwa mashine ya kuchapisha. Viage hivi vinatengenezwa kwa wingi sana katika nchi mbalimbali.

Kuna aina kuu mbili za vigae/tiles hizi za kutengeneza ambazo ni

  1. Vigae/tiles za ceramic
  2. Vigae/tiles za porcelain

Aina hizi za viage/tiles za kutengeneza zinafanana sana kwa vitu vingi, kuanzia malighafi za kuzitengeneza mpaka utengenezaji wenyewe lakini kuan vitu vinavyozitofautisha.

Tofauti kati ya vigae/tiles za ceramic na vigae/tiles za porelain.

-Vigae/tiles za ceramic ni rahisi kupitisha maji na havifai sana maeneo yenye maji maji sana wakati vigae/tiles za porcelain ni vizito na vinadumu zaidi.

-Utengenezaji wa vigae/tiles za ceramic unahusisha matumizi ya pressure ya kiwango cha chini na joto la kiwango cha chini kwenye malighafi zake ndani ya mashine wakati utengenezaji wa vigae/tiles za porcelain unahusisha matumizi ya pressure ya kiwango cha juu na joto la kiwango cha juu pia na kwa muda mrefu zaidi.

-Vigae/tiles za ceramic zinatengenezwa kwa kutumia malighafi ya mchanganyiko wa udongo wa earthen, mfinyanzi pamoja na maji wakati tiles za porcelain zinatengenezwa kwa malighafi ya mchanganyiko wa udongo wa earthen, mfinyazi, feldspar, silica na maji.

-Vigae/tiles za ceramic ni laini ukilinganisha na vigae/tiles za porcelain ambazo ni ngumu zaidi.

-Vigae/tiles za ceramic zinapitisha maji kwa 3% wakati vigae/tiles za porcelain zinaweza kupitisha kwa 0.5% hivyo porcelain ni kama hazipitisha kabisa maji kwa sababu zikishatengenezwa hujaribiwa kwa kutukumbukizwa ndani ya maji na ikiwa kigae/tile hiyo imenyonya maji kwa zaidi ya 0.5% basi moja kwa moja inapoteza sifa ya kuwa kigae/tile ya porcelain.

-Vigae/tiles za ceramic hazidumu muda mrefu ukilinganisha na vigae/tile za porcelain ambazo zinadumu sana.

-Vigae/tiles za ceramic haziruhusu kabisa mwanga wakati vigae/tiles za porcelain zinaruhusu mwanga kidogo kupita.

 -Kigae/tile ya ceramic ukiiangusha kwenye sakafu haiwezi kutoa mlio kama wa kengele wakati ukiangusha kigae/tile ya porcelain sakafuni inatoa mlio kama wa kengele.

-Vigae/tiles za ceramic ni nyepesi kidogo ukilinganisha na vigae/tiles za porcelain ambazo ni nzito zaidi.

-Vigae/tiles za ceramic zinavunjika kiurahisi zaidi ukilinganisha na vigae/tiles za porcelain ambazo ni ngumu zaidi kuvunjika.

-Ni rahisi zaidi kusafisha vigae/tiles za porcelain kwa sababu hazinyonyi maji san ana kuzifubaza wakati kusafisha vigae/tiles za ceramic ambazo zinanyonya maji zaidi na rahisi kufubaza vigae/tiles hizo.

-Vigae/tiles za ceramic ni dhaifu zaidi ukilinganisha na vigae/tiles za porcelain ambazo ni imara zaidi.

-Ikiwa imetokea moto vigae/tiles za ceramic zinashika moto kiurahisi ukilinganisha na vigae/tiles za porcelain ambazo zina uwezo mkubwa zaidi wa kuzuia moto kuendelea.

-Vigae/tiles za ceramic zinaweza kukatwa kiurahisi ukilinganisha na vigae/tiles za porcelain ambazo ni ngumu zaidi kuzikata.

-Ujenzi au ufitishaji wa vigae/tiles za ceramic ni rahisi na haraka wakati ujenzi au ufitishaji wa vigae/tiles za porcelain ni mgumu zaidi, unachukua mud ana nguvu kazi kubwa kukamilisha.

-Vigae/tiles za ceramic zikiharibika ni vigumu kufanya marekebisho kwenye sehemu iliyoharibika wakati vigae/tiles za ceramic ni rahisi zaidi kufanya hivyo.

-Vigae/tiles za ceramic zinadumu muda mchache zaidi ukilinganisha na vigae/tiles za porcelain ambazo zinadumu miaka mingi sana.

-Vigae/tiles za ceramic zinashauriwa kutumika maeneo ya ndani na hasa kwenye kuta ambazo hazilowi maji mara kwa mara pamoja na maeneo yasiyokanyagwa sana kama vile vyumbani wakati vigae/tiles za porcelain zinashauriwa kuwekwa maeneo yanayokanyagwa sana kama vibarazani na maeneo ya nje pamoja na maeneo yenye unyevu mwingi na yanayolowa kama mabafuni na kwenye swimming pools.

-Vigae/tiles za ceramic zinauzwa kwa gharama nafuu ukilinganisha na vigae/tiles za porcelain ambazo ni ghali zaidi.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call 255717452790

Kupata makala bora za ujenzi tembelea website yetu kila siku www.ujenzimakini.com

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *