PAA LA VIGAE VYA LAMI NA MCHANGA (ASPHALT SHINGLES ROOF)
-Paa la Vigae vya mchanganyiko wa lami na mchanga wakati mwingine huchanganywa pia na mawe madogo madogo, maarufu kwa jina la kitaalamu kama (asphalt shingle roof) ni aina ya vigae ambavyo vimetokana na ubunifu wa kisasa wa watalaamu. Ni aina ya vigae vilivyotengenezwa kwa malighafi kama ya mpira lakini vinakatwa vizuri na kuwa na mwonekano kama wa vigae vya udongo au mawe.
FAIDA ZA PAA LA VIGAE VYA LAMI NA MCHANGA (ASPHALT SHINGLE ROOF)
-Paa la vigae vya mchanganyiko wa lami na mchanga vina gharama nafuu sana, licha ya kwamba havidumu muda mrefu sana ukilinganisha na aina nyingi za vigae, kwa kutozidi miaka 20 lakini gharama yake pia ni ndogo sana ukilinganisha na aina nyingine za vigae.
-Paa la vigae vya lami na mchanga vinapatikana katika aina na rangi mbalimbali kiasi cha kuendana na kila aina ya ubunifu wa jengo husika.
-Paa la vigae vya lami na mchanga lina urahisi mkubwa sana katika kuezeka na linatumia muda mfupi sana kukamilika kutegemea na ukubwa wa kazi yenyewe.
-Paa la vigae vya lami na mchanga ni aina ya paa ambalo ubora wake unaendana sana na beo yake hivyo watu wengi hupendelea kwa sababu inawarahishia sana kazi watu ambao wanahitaji kitu kisicho cha gharama sana lakini kinaweza kufanya kazi kwa miaka ambayo inawatosha kabla hawajafanya ukarabati na kubadili au kuachana na mradi husika.
CHANGAMOTO ZA PAA LA VIGAE VYA LAMI NA MCHANGA.
-Paa la vigae vya lami na mchanga vina changamoto ya kushindwa kuhimili maeneo yenye joto kali ambapo mara nyingi rangi yake hufubaa au kupata mipasuko.
-Paa la vigae vya lami na mchanga pia hushindwa kuhimili maeneo yenye mabadiliko makubwa ya hali ya hewa kama vile misimu ya joto kali kasha misimu ya baridi kali kwani hupelekea mipasuko pia.
-Paa la vigae vya lami na mchanga sio rafiki mzuri wa mazingira kwani hutengenezwa kutoka kwenye malighafi iliyochanganyika na mafuta ya petrol, pia utengenezaji wake unahusisha matumizi makubwa sana ya nishati viwandani ambayo yanachangia sana katika uharibifu wa mazingira.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!