NAMNA YA KUZUIA UVUJAJI WA MAJI KWENYE PAA, BARAZA AU SAKAFU YA JUU.

-Kuzuia maji yanayotokea kwenye paa, concrete gutter, baraza au sakafu ya juu ni changamoto inayohitaji umakini, ubunifu na mbinu ya ziada kutokana na kwamba baraza au sakafu hizi ziko flat na maji husogea taratibu sana hivyo kupata muda wa kutosha kuingia kwenye zege na kuanza kuvuja. Katika maeneo yanayopita maji mara nyingi huwa na mifereji midogo inayokusanya maji hayo na kuyapeleka kwenye bomba zilizosimama wima(vertical ducts) ambazo huyashusha chini, mifereji hii pia mara nyingi huwa chanzo cha maji kuvujia kwenye kuta au sakafu.

UKUTA UNAOVUJISHA MAJI

-Kadiri sakafu inavyokuwa na mteremko mkali zaidi ndivyo kadiri inavyokuwa salama dhidi ya maji kuvuja kwani mteremko huruhusu maji kukimbia kwa kasi kabla ya kuzama kwenye zege. Pia sakafu ambayo ni rafu ina nafasi kubwa ya kuvujisha maji kuliko sakafu ambayo imefanyiwa finishingi.

-Njia nyingine ya kuzuia maji kuvuja kwenye jengo ni kwa kutumia vifaa vya kimiminika na kemikali kama vile (concrete filler and sealant) kuziba maeneo ambayo yanavuja kama kutakuwa na nyufa ndogo au kubwa zinazopelekea maji kuvuja.

KUTANDAZA ZULIA MAENEO YENYE UDHAIFU, MIPASUKO AU MATUNDU

-Njia bora kabisa ya kuzuia maji kuvuja kwenye kuta au baraza za juu ni kwa kutumia zulia la plastiki maarufu kama “waterproofing membrane”.  Zulia hili ni jembamba na linatandazwa eneo lote la juu la sakafu husika. Juu ya zulia hilo la plastiki maarufu kama “waterproofing membrane” yanamwaga material mithili ya zege inayojulikana kama “concrete filler and sealant” au zege yenyewe ambayo itamwagwa katika umbo la kutengeneza mteremko utakaopeleka maji kwenye matundu(ducts) yaliyosimama wima ambayo yanashusha maji hayo chini. Mwisho unaweza kumalizia kwa finishingi au kuweka urembo kama vigae vya sakafuni(tiles) n.k.,

SAKAFU ILIYOKARABATIWA NA KUFANYIWA FINISHINGI UPYA

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *