STOO YA MAJI YA ZIMAMOTO(FIRE STORAGE TANKS)

Kiasi cha maji ya zimamoto katika Matangi ya maji ya kuzimia moto kinaamuliwa na kiasi cha hatari ya mradi husika au jengo husika linalolengwa.

Kuna Aina Tatu za Viwango vya Hatari za Moto

-Hatari ndogo (kama mashule, nyumba za kuishi na maofisi)

-Hatari ya kawaida (kama vile viwandani na maofisini)

-Hatari kubwa (maeneo yanayohifadhi vitu vinavyoshika moto kwa haraka kama viwanda vya ndege, viwanda vya rangi na kemikali mbalimbali)

Matangi Yanayotumika Kuhifadhi Maji Ya Kuzima Moto Yanayochimbiwa Chini Ardhini

Utaratibu wa zimamoto unaweka kila jengo kuangukia kwenye moja ya aina ya hizo hatari tatu tofauti. Kiasi cha maji kinachohifadhiwa kinatokana na idadi ya masaa ambayo maji hayo yataendelea kuzima moto mpaka yatakapokatika. Ukubwa wa Matangi hayo ya maji ndio huwekwa na kuamua idadi ya masaa ambayo yatamwagika. Utaratibu wa zimamoto kwa majengo unaweza kuweka kwenye majengo yenye hatari ndogo maji yakamwagika kwa lisaa limoja na yenye hatari kubwa ikachukua hata masaa manne.

Tangi La Kuhifadhiwa Maji Ya Kuzima Moto Katika Jengo Likichimbiwa Chini Ardhini

Kwa kawaida maji huhifadhiwa kwenye matangi ya zege yaliyochimbiwa chini ya ardhi. Ni muhimu kuzingatiwa kwamba maji haya yanayohifadhiwa yanakuwa yamejaa muda wote na hayatumiki kwa matumizi mengine yoyote zaidi ya kuzima moto. Matangi hay ani tofauti na Matangi ya kuhifadhia maji kwa matumizi ya majumbani. Wataalamu husika wanapaswa kuhakikisha kwamba maji haya hayaharibiki kwa namna yoyote na kushindwa kutoa huduma iliyokusudiwa.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *