GHARAMA ZA ZIADA ZA MICHORO YA RAMANI

Tunapolipia gharama za huduma za kitaalamu watu wengi huwa hatujui hasa tunalipia nini.  Mara nyingi tunafikiri kwamba nahitaji huduma fulani ya kitaalamu kama vile ushauri kuhusu afya na maelekezo mengine au nahitaji ushauri kuhusu ujenzi na michoro ya ujenzi lakini hatujui kile hasa tunacholipia. Hivyo nitafafanua hapa chini.

TUNAFAHAMU KWAMBA TUNAHITAJI HUDUMA ZA UJENZI LAKINI HATUJUI HASA TUNALIPIA NINI

-Kwanza kabisa huwa tunalipia utaalamu wenyewe, yaani mtu anayekupa huduma ya kitaalamu ametumia gharama kubwa na kujitoa miaka mingi kujifunza na kujenga uwezo na uzoefu na kuweza kutoa huduma sahihi kwa eneo husika hivyo anatumia uwezo wake huo kukupa huduma yenye ubora na itakayokuwa na manufaa makubwa kwako, kwa hiyo tunamlipa kwa utaalamu wake huo.

TUNALIPIA UTAALAMU NA UZOEFU

-Pili tunalipia muda, hapa mtu mwenye utaalamu fulani anaacha mambo yake yote, anaacha kazi zake na kazi za wengine, anaahirisha shughuli zote za kijamii na kazi nyingine za kumuingizia kipato anashughulika na kazi yako au jambo lako. Huu muda ambao anautumia kwa kazi yako ni muda ambao angekuwa anafanya kazi nyingine ambapo ameiacha kazi hiyo ili afanye kazi yako.

TUNALIPIA MUDA

-Jambo la mwisho ni kwamba tunalipia ubora, hapa kwenye kulipia ubora ndio kunakoleta utofauti kati ya mtu mwenye utaalamu na uzoefu mkubwa na mtu asiye na utaalamu na uzoefu kwa sababu gharama ya huduma zao itakuwa na utofauti mkubwa ambapo kama wewe ni mtu unayethamini kitu chenye thamani kubwa utakuwa tayari kufanya kazi na mtu mwenye uwezo na uzoefu zaidi hata kama itakubidi kumlipa zaidi.

TUNALIPIA UBORA

Sasa kwenye ujenzi kuna kitu huwa kinaitwa “variation”, kwa maana ya kwamba ni mabadiliko ya gharama pale inapotokea mabadiliko kwenye ujenzi. Kwenye huduma ya michoro ya ramani napo kuna hiyo “variation” ambayo ni ongezeko la gharama ambalo hutokea wakati kazi ya michoro ikiwa imeshafanyika lakini kabla ya kutengeneza michoro ya mwisho yanatokea mawazo mbadala ambayo yanasababisha kuhitaji mabadiliko ya michoro ambayo yanalazimu sehemu ya kazi hiyo kurudiwa. Sehemu ya kazi inaporudiwa ile kanuni ya utaalamu na muda inakuwepo tena kwa maana ya kwamba inachukua muda zaidi na kuhitaji utaalamu pia, hivyo inalazimu kuwepo kwa ongezeko la gharama “variation”.

MABADILIKO YA MICHORO YA RAMANI YANAPELEKEA PIA ONGEZEKO LA GHARAMA ZA MICHORO

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *