MABADILIKO WAKATI UJENZI UNAENDELEA YASIFANYIKE KIHOLELA

Mara nyingi sana hasa kwa miradi ya watu binafsi wakati ujenzi ukiwa unaendelea hujitokeza mawazo mbadala ya mabadiliko ya jengo ambayo huonekana ni muhimu sana kwa mteja, hivyo kutakiwa kuingizwa kwenye utekelezaji. Mabadiliko ni jambo zuri hasa yanapokuwa yameamuliwa na mtumiaji wa jengo lakini changamoto inayojitokeza ni kwamba huwa yanaamuliwa kiholela bila kumshirikisha mtaalamu aliyefanya michoro husika na hivyo kuharibu ubora na usahihi wa kazi ya usanifu kwa sababu aidha mtaalamu hayupo saiti kwa wakati huo haya maamuzi yakifanyika au hayupo kabisa kwenye ujenzi wa mradi husika kwa sababu.

MPANGILIO WA KIMATUMIZI NA KIMUONEKANO WA JENGO UNA KANUNI ZAKE KITAALAMU

-Kwanza kabisa suala la ubunifu na mpangilio wa kimatumizi na kimuonekano wa jengo una kanuni zake kitaalamu na kila kitu kinawekwa eneo fulani kwa sababu maalum na ya msingi, lakini inapokuja mabadiliko ya kiholela kwa sababu yanafanywa na watu wasio na uelewa sahihi wa kanuni za mipangilio hufanya maamuzi kiholela na kupelekea uharibifu wa kimpangilio hasa wa kimatumizi na kimuonekano. Makosa haya yote hufanyika huku wanaofanya wakiwa hawajui kabisa kwamba wanakosea kitu kinachopelekea wao kujiamini na kuendelea na maamuzi hayo.

WATU WASIO NA UTAALAMU WAKIFANYA MAAMUZI YANAYOHITAJI UTAALAMU HUFANYA MAKOSA BILA KUJUA KWAMBA WANAFANYA MAKOSA

-Athari nyingine ya kufanya mabadiliko kiholela bila kumshirikisha mtaalamu aliyefanya ubunifu husika ni kuharibu uelekeo sahihi wa jengo. Ikiwa kuna baadhi ya vyumba au matumizi mengine vitakavyoondolewa kwenye nafasi zake au kuongezwa kwa vitu ambavyo havikuwepo kunaweza ambapo kutahama na visasili vyako na kuharibu au kuondoa umuhimu wa uelekeo wa jengo uliowekwa na mtaalamu aliyefanya ubunifu.

KUFANYA MABADILIKO KIHOLELA HUPELEKEA KUDHOOFISHA UIMARA WA JENGO

N:B Kufanya mabadiliko kiholela mara nyingi hupelekea pia kudhoofisha uimara wa jengo hasa kama jengo lenyewe ni la ghorofa.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *