UMUHIMU WA KUWEKA KUTA ZA VIOO KWENYE ENEO LA KUOGA “SHOWER CLOSURE” BAFUNI.
Kwa staili ya kisasa kwa sehemu kubwa eneo la bafuni ni eneo la wazi ambapo huwa na vitu vingi ambavyo mtu anayeingia maliwato anavitumia kama vile sinki la kunawia mikono(handwash basin), sinki la wc, jaccuzi, bathtub, eneo la shower n.k., hivyo licha ya kwamba vitu hivi wakati mwingine mara chache vinaweza kutengwa kwenye vyumba tofauti au kuwekewa mpaka na ukuta lakini bado umuhimu wa kuweka kuta za vioo kwenye eneo la kuogea maarufu kama “shower closure” ni muhimu sana kwa sababu zifuatazo.
-Bafu la kuta za vioo(shower closure) linasaidia kuzuia maji kutawanyika na kulowesha bafu nzima pamoja na maeneo mengine hivyo yale maji maji yanaleta hali ya kutojisikia vizuri mtu anapokuwa bafuni.
-Bafu la kuta za vioo(shower closure) linasaidia bafu kuwa safi muda mwingi kwa kuepusha unyevu unaoshika uchafu na kuugandisha hivyo kusababisha uchafu ulionata unaotakiwa kuondolewa kwa kusuguliwa sana.
-Bafu la kuta za vioo(shower closure) linaongeza sana hadhi ya bafu na maliwato kwa ujumla kwani vile vioo na muundo wake huleta mtazamo wa picha wa hadhi ya juu.
-Bafu la kuta za vioo(shower closure) linasaidia kutenga sehemu maalum ya bafu kwa ajili ya kuogea tofauti na bafu lisilo na “shower closure” ambapo mtu anaweza kusimama popote na kutawanya maj bafu zima jambo linalokuwa hatari kwani inapelekea utelezi ambao unaweza kusababisha hata tu kuumia.
-Bafu la kuta za vioo(shower closure) linapendezesha sana bafu kwani satili na mpangilio wake wa vioo sambamba na zile “mixer” zake za aina tofauti tofauti huwa na mvuto wa kipekee na wa aina yake.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!