CHANGAMOTO ZA UJENZI WA HARAKA(FAST TRACK CONSTRUCTION).
-Kufanya kazi kwa wakati mmoja kwa eneo moja, kwa watu wa fani mbalimbali kunaongeza hatari ya watu kupata ajali katika eneo la ujenzi hivyo kujahitajika umakini mkubwa katika kupangilia watu wa fani zote ambao kila mtu atakuwa anafanya kazi yake kupunguza hatari ya ajali na watu kuumizana.
-Ikiwa mkandarasi husika hana uzoefu mkubwa wa miradi hii ya ujenzi wa haraka, anaweza kuchelewesha kazi na kushindwa kukamilisha kazi hizi za ujenzi wa haraka kwa wakati na hivyo kujikuta akikutana na adhabu nyingi na za pamoja za kushindwa kumaliza kazi kwa wakati uliopangwa n ahata kumuathiri katika eneo la usimamizi wa fedha katika mradi.
-Kama mkandarasi wa mradi husika hana uzoefu wa ujenzi wa haraka mradi husika unaweza kuwa na makosa mengi kutokana na uduni wa mawasiliano na usimamizi ambavyo vitakuwa vinahusisha watu wa fani mbalimbali pamoja na wakandarasi wadogo wasaidizi katika mradi.
NB: Ujenzi Wa Haraka Unahitaji Watu Wenye Uwezo Mkubwa Kwa Aina Hii Ya Miradi na Uzoefu Pia, Unaweza Kuwasiliana Nasi Ikiwa Una Uhitaji wa Huduma Hii Ya Ujenzi Wa Haraka Tutakupatia Watu Sahihi Ili Kuepuka Changamoto Zote Zinazoweza Kusababishwa na Aina Hii Ya Miradi Ya Ujenzi wa Haraka
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!