MIFUMO YOTE INAYOSAMBAZA HUDUMA NDANI YA JENGO HAIPASWA KUONEKANA KWA NJE.

Muonekano wa jengo kwa nje, kwa ajili ya mvuto na muonekano bora haupaswi kuwa na vipengele vingine vyovyote zaidi ya vipengele vya kisanifu vilivyopangiliwa kwa ustadi mzuri kwa ajili ya kuboresha muonekano na kuleta maana inayokusudiwa ya jengo husika.

MIFUMO INAYOSAMBAZA HUDUMA NDANI YA JENGO INAPASWA KUPITA SEHEMU MAALUMU PEKE YAKE

Kumekuwepo na changamoto kubwa kwenye eneo hili zinaletwa na mifumo inayohusika na kusambaza huduma muhimu katika jengo kama vile mifumo ya umeme, mifumo ya zima moto, mifumo ya maji safi, maji taka, mifumo ya mitandao, televisheni na vitu vingine ambavyo vimekuwa vikipachikwa kwa nje na kuanza kuleta muonekano na maana tofauti ya jengo husika.

MIFUMO INAYOSAMBAZA HUDUMA NDANI YA JENGO INAPOKAA NJE YA JENGO INAHARIBU MUONEKANO NA KUPOTEZA MAANA ILIYOKUSUDIWA KISANIFU

Hili limekuwa likipelekea kuharibu na hata kuleta usumbufu kwa muonekano wa nje wa jengo, lakini hata hivyo kukiwa na njia mbadala wa kulitatua sio kwa kuhamishia mifumo hii kuonekana kwa ndani bali kuijengea njia zake zenyewe ambazo haitaonekana wala kuleta utofauti wowote wa kimuonekano kwa nje wala kwa ndani na hivyo kutoharibu ubora, uzuri na maana ya muonekano wa jengo.

MUONEKANO WA JENGO UNAPASWA KUWA RAHISI INAVYOWEZEKANA ISIPOKUWA TU KWA VIPENGELE VYA UREMBO AU MAANA NYINGINE YA JENGO

Mara nyingi njia bora zaidi inayotumika kuhifadhi mifumo na njia za kupitisha mifumo inayosambaza huduma zote muhimu katika jengo ni uwepo wa “mifereji wima(ducts)”, ambayo imejengwa kama nafasi ndani ya nguzo iliyosimama wima inayosafirisha huduma zote hizi ndani ya jengo.

NJIA ZOTE ZINAZOTUMIKA KUSAMBAZA HUDUMA ZINATAKIWA KUFICHWA NDANI YA MIFEREJI WIMA(DUCTS) AMBAYO NAYO INATAKIWA KUWA NDANI YA JENGO ISIONEKANE KWA NJE.

Kwa kufanya hivi muonekano wa jengo unabaki na muonekano rahisi na kuleta maana iliyokusudiwa kisanifu na kitalaamu.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *