TENGENEZA BUSTANI NZURI KUONGEZA THAMANI YA NYUMBA NA MANDHARI YAKE.
Utengenezaji wa bustani kwa sababu za mbalimbali ikiwemo kuboresha na kupendeza mazingira ni jamba ambalo limekuwa likifanyika tangu zamani za kale. Mpangilio wa kujenga mistari ya mawe(kerbstones) na vigae vya tofali za ardhini(paving blocks) kama ardhi ngumu pamoja na upandaji miti kwa mpangilio sahihi uliotengenezwa kwenye ramani huongeza mvuto na thamani ya nyumba na mandhari yake kwa kiasi kikubwa sana.
Mandhari inayozunguka nyumba hujumuisha maeneo yenye ardhi ngumu(hard landscape) kama vile njia za gari na za miguu, parking za gari, eneo la kupumzika maarufu kama “gazebo” n.k., ardhi laini(soft landscape) ambayo hujumuisha maeneo yenye bustani za nyasi, maua, miti ya kivuli, miti ya matunda, mbogamboga na maeneo mengine yote yenye kijani kibichi, maji(water landscape) ambayo hujumuisha bwawa la kuogelea(swimming pool), bwawa la samaki, mifereji ya umwagiliaji, maji yanayoruka n.k.,. Mjumuiko wa haya katika mpangilio sahihi wa eneo la kiwanja linalozunguka nyumba huongeza sana thamani ya nyumba na kuboresha sana mandhari inayozunguka nyumba.
Jambo la muhimu sana ni kwamba yote haya yanapaswa kuanza na michoro ya ramani kabla ya utekelezaji. Unapotanguliza utekelezaji kabla au bila ya michoro ya ramani ya bustani na mandhari yote ya nyumba pamoja na mahusiano yake na nyumba yenyewe unajiandaa kukutana na changamoto sana na mwisho wa siku ubora wa kazi utakuwa wa viwango vya chini sana tofauti na ikiwa utaanza na ramani au pengine ukafeli kabisa.
Tumia bustani na mpangilio sahihi wa mandhari inayozunguka nyumba kuongeza sana thamani ya nyumba yako.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Misaada wa tamani nzuri ya bustani iyanzie kwenye geti
Karibu sana kaka.
Whatsapp +255717452790.
Ni umbali Gani unatakiwa kuzingatia kutoka ukutani Hadi sehemu ambayo unatakiwa kuanza kupnda maua
Tuwasiliane +255 717 452 790.