KUPIGA JENGO PLASTA AU RIPU

Kupiga jengo ripu maarufu kama kupiga plasta ni kitendo cha kulipaka jengo zege laini ambalo ni mchanganyiko wa saruji na mchanga ili kusawazisha uso wake kwa kufukia na kusawazisha maeneo yote ambayo hayajanyooka vizuri au kukaa sawa wakati wa kujenga tofauli za kuta na nguzo. Lengo kuu la kupiga plasta ni kusawazisha uso katika “level” moja ili kuliandaa kwa ajili ya kazi za umaliziaji(finishing works). Shughuli za umaliziaji katika kulifikisha jengo kwenye muonekano wenye mvuto ni kama vile kupiga nyeru(skimming) na kisha kupaka rangi(painting). Hizi ni hatua za mwisho katika kutengeneza uso mzuri wa jengo unaovutia ambazo haziwezi kufanyika kabla ya kupiga ripu itakayoandaa uso laini wa jengo tayari kwa kuuboresha zaidi.

KUPIGA PLASTA AU RIPU NI KAZI INAYOTAKIWA KUFANYIKA KWA UMAKINI MKUBWA ILI KAZI YA UMALIZIAJI IWEZE KUWA KATIKA VIWANGO BORA

Ili kazi ya kupiga ripu/plasta ifanyika kwa urahisi, kwa ufanisi na hata kwa gharama ya wastani wa kawaida inabidi kazi zinatangulia za kujenga nguzo na kuta ziwe zimefanyika kwa usahihi mkubwa, ikiwa kazi hizi hakufanyika kwa ufanisi unaotakiwa kazi nzima ya kupiga jengo huwa inakuwa ngumu, kubwa na inayohusisha gharama kubwa sana ili kuweza kulirudisha jengo katika hali nzuri. Umakini mkubwa kuanzia kwenye kulipanga jengo ndani ya msingi(setting out) kisha kutumia vipimo na vifaa vizuri vya kunyoosha na kuzingatia pembe zote na vipimo sahihi pamoja na ufundi bora ambao utapangilia kila kitu katika usahihi mkubwa pamoja na vifaa vya ujenzi kama vile tofali zenye viwango bora sana na zenye ukubwa unaolingana. Kwa kuzingatia haya kazi ya kuja kupiga jengo ripu/plasta inakuja kuwa nzuri, rahisi na yenye ufanisi mkubwa.

KAZI YA KUPIGA PLASTA HUWA RAHISI KAMA KAZI ZILIZOTANGULIA ZILIFANYIKA KWA USAHIHI

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

2 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *