KUJENGA NYUMBA YA KISASA BILA USIMAMIZI WA KITAALAMU NI KUIHUJUMU NYUMBA.

Ni kati ya mambo yanayoshangaza sana jinsi gharama za vifaa vya ujenzi zilivyo kubwa lakini bado kutokana na kuongozwa na hisia watu wanaogopa zaidi gharama za usimamizi wa kitaalamu kuliko gharama za vifaa vya ujenzi bila kujali umuhimu mkubwa sana wa huduma za usimamizi wa kitaalamu katika jengo. Unaweza kushangaa jinsi mtu anaweza kuwa tayari kununua vifaa vya gharama kubwa tena vya ghali kwa wingi na kwa haraka katika ujenzi lakini hayuko tayari kuhakikisha ujenzi husika unasimamiwa na mtu mwenye uwezo mkubwa katika usimamizi wa mradi wa ujenzi husika.

UMUHIMU WA VIFAA BORA KATIKA UJENZI UNA UZITO SAWA NA UMUHIMU WA HUDUMA BORA ZA USIMAMIZI WA UJENZI

Huduma bora za usimamizi wa mradi wa jengo katika ujenzi ndizo zinazoleta matokeo yenye ubora katika ujenzi na sio vifaa vyenye ubora peke yake. Kununua vifaa vyenye ubora ni vizuri sana lakini hapo unakuwa umefanya nusu ya kazi ya kuhakikisha jengo lako linakuwa katika viwango bora lakini bado umepuuza nusu nyingine ya kazi ya kuhakikisha unafikia ubora unaoutaka kwa kuhakikisha unaajiri viwango bora vya usimamizi ambao utakuwa sehemu muhimu ya kufanya maamuzi sahihi na kuyasimamia.

UBORA WA JENGO NI MCHANGANYIKO WA VIFAA BORA NA HUDUMA BORA

Hivyo usikimbilie tu kununua vifaa vyenye ubora ukafikiri umemaliza na utafanikisha kupata jengo lenye ubora kwa kufanya hivyo peke yake, huo ni upande mmoja pekee wa kazi nzima ya kufanikisha ubora wa jengo lako, hapo bado utahitaji pia usimamizi bora wa uhakikisha vifaa hivyo vinajengwa katika viwango sahihi vya ubora na kwa mpangilio sahihi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *