MADIRISHA YA ALUMINIUM NA MADIRISHA YA PVC

Madirisha ya aluminium ni aina ya madirisha yanayotengenezwa kwa kutumia malighafi ya aluminium katika fremu yake na katika ya dirisha(window panel) kunakuwa na kioo. Madirisha ya PVC ni aina ya madirisha yanayotengenezwa kwa malighafi fulani ya plastiki kwenye fremu yake wakati katikati ya dirisha husika(window panel) kuna kuwa na kioo.

DIRISHA LA PVC

Aina hizi za madirisha japo kwa mbali zinaonekana kukaribia kufanana lakini kiuhalisia kuna utofauti mkubwa. Madirisha ya pvc ni imara zaidi, yenye mvuto zaidi, ya hadhi ya juu zaidi na gharama yake ni kubwa sana ukilinganisha na madirisha ya aluminium wakati madirisha ya aluminium japo ni imara pia lakini hayana uwezo mkubwa kama madirisha ya pvc na gharama yake ni nafuu zaidi ukijaribu kulinganisha na madirisha ya pvc.

DIRISHA LA ALUMINIUM

Madirisha ya pvc ni ya hadhi ya juu zaidi na mara nyingi hupatikana zaidi katika rangi nyeupe na yanayong’aa sana wakati madirisha ya aluminium mara nyingi hupatikana katika rangi tatu kuu rangi ya fedha, rangi nyeupe na rangi ya bronzi. Kwa mtu asiyejua vizuri anaweza kushindwa kutofautisha kati ya dirisha la aluminium nyeupe na dirisha la pvc kwani kuna ufanano mkubwa ukiangalia juu, hata hivyo aluminium nyeupe ni ya gharama zaidi kuliko aluminium za rangi nyingine. Kwa hivyo kama mtu una uwezo mzuri kifedha naweza kushauri kwamba dirisha la pvc ni lenye ubora zaidi na thamani zaidi kwani hata kudumu linadumu zaidi vinginevyo madirisha ya aluminium ni mazuri sana pia, yanapatikana kwa wingi sana na bei ni nafuu zaidi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

1 reply

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *