JENGO LA BIASHARA LAZIMA LIVUTIE KIMUONEKANO.

Kuna msemo maarufu wa kiingereza unasema “don’t judge a book by it’s cover”, ukimaanisha “usihukumu kitabu kwa muonekano wake wa nje”, sasa kama mtu hujui asili ya binadamu msemo kama huu unaweza kukupoteza ukifikiri watu huwa wanajihangaisha kufahamu undani wa kitu. Watu wengi huwa hawajihangaisha sana kufahamu undani wa kitu chochote huwa wanaishia kuhukumu kwa kiasi wanachoona. Sasa hapa linapokuja suala muonekano wa jengo lako, kama unahitaji lionekane ni lenye thamani kubwa na ambalo watu wanaweza kuwa tayari kulipa kiasi kikubwa cha fedha kupanga au hata kununua ikiwa unauza basi moja kati ya mambo ya kuzingatia sana ni muonekano wake wa nje kwa sababu hicho ndicho kitu watu wanaona na kuhukumu, hata wale wachache ambao watafanikiwa kuingia ndani ya jengo wataanza kwanza kuliona kwa nje kwa hiyo tayari watakuwa wameanza kupata hisia hasi au chanya kabla hivyo hata wakiingia ndani kile walichokiona nje kitakuwa kimeshakuwa sehemu ya mtazamo wao kwa namna watahukumu ndani.

MVUTO WA KIMUONEKANO WA NJE NI ISHARA ZA MWANZONI ZA UZURI WA JENGO KWA NDANI

Hivyo ni muhimu sana kuhakikisha kwamba jengo lako linavutia sana kimuonekano kwa kufanya kazi ya “design” ambayo ni nzuri na ya kipekee ambayo imepangiliwa kwa umaridadi na kwa ubinifu wa hali ya juu na kwa usahihi wa kimtirirko. Kisha utahitaji jengo lenyewe pia lijengwe vizuri kwa ustadi na kwa ufundi wa viwango vya juu likisimamiwa na mtaalamu anayehakikisha kila kitu vinachangia kwenye uzuri wa muonekano kinakuwepo na kinawekwa katika sehemu sahihi iliyopangwa kwa viwango sahihi na kwa ukubwa unaolandana vizuri na vipengele vingine vinavyoshibanisha kimoja na kingine kufikia ule umaridadi na mpangilio uliokusudiwa kufikiwa tangu unapangwa kwenye akili ya msanifu mbunifu wa jengo.

MVUTO WA NJE NI MATOKEO YA MPANGILIO BORA WA JENGO KWA UJUMLA NA UBUNIFU MKUBWA KATIKA KUFANYA

Hili litafanyika vizuri na kwa viwango vikubwa ikiwa utachagua wataalamu sahihi wa ushauri wa kitalaamu sambamba na wajenzi wanaoshirikiana nao tangu mwanzoni kabisa mwa kazi na kuazimia mamoja.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *