MPE KAZI YA UJENZI MTU ALIYEFANYA MIRADI YA VIWANGO VYA JUU VYA UBORA.

Linapokuja suala la ujenzi watu wengi husikiliza watu wa karibu au watu wanaofahamiana nao kuambiwa mtu fulani anafanya kazi nzuri mpe kazi na kwa kutumia ushawishi wa mazungumzo na maneno watu wamekuwa wakitoa kazi kwa namna hiyo. Ni kawaida na ni asili ya binadamu mtu kumwamini mtu pale anapopendekezwa na mtu mwingine anyemfahamu, na ni vizuri kusikia watu wanamzungumziaje mtu huyo lakini kusikiliza peke yake na kutoa kazi kwa mtu husika ni sawa na kucheza Kamari. Kwa bahati mtu huyo anaweza akawa kweli ana uwezo lakini pia unaweza kukuta hata huyo anayempendekeza anaweza kuwa naye amesikia tu habari zake na hajui uwezo halisi wa mhusika na yanayosemwa kuhusu yeye yakawa hayana uhalisia.

UWEZO NA UZOEFU WA MTAALAMU HULETA UHAKIKA WA MATOKEO BORA KATIKA UJENZI

Hivyo unapofikiria kumpa mtu kazi ni vyema na muhimu sana katika kujihakikishia kwamba kazi itafanyika katika viwango vya juu na sio kubahatisha na kujikuta kwenye upande wa hasara, uanze kwanza kwa kutaka kufahamu kazi zilizofanywa na mhusika kujua viwango vya ubora na umakini vya mhusika. Hii itasaidia sana katika kupunguza hatari ya kusumbuana na watu katika ya kazi na hata kujikuta ukipoteza muda na gharama. Muhimu ni kuwa wazi kabisa mwanzoni kwamba utahitaji uone kazi kadhaa zilizofanywa na mhusika kwanza na kuzitathmini ndio kuweza kutoa kazi na hasa ujihakikishie kwamba kazi hizo zimefanyika chini ya usimamizi wake.

KUFAHAMU UWEZO WA MTAALAMU KUPITIA KAZI ZA UJENZI ALIZOFANYA MWENYEWE KUTAKUEPUSHA AU KUKUPUNGUZIA HATARI ZISIZOTARAJIWA.

Hiyo ni njia sahihi, salama na ya uhakika kabisa kwamba kazi yako itafanyika katika viwango hivyo nap engine hata zaidi kama kutakuwa na mpango kazi ulioandaliwa kwa usahihi mkubwa.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *