MSIMAMIZI MKUU WA UJENZI ATENGENEZE MWONGOZO, UTAKAOFUATWA NA WASAIDIZI YEYE ANAPOKOSEKANA.

Mradi wa ujenzi unapokuwa katika hatua ya ujenzi huhusisha mambo mengi sana, wote tunajua kwamba karibu kila kitu kinachohusika kwenye mradi wa ujenzi ni cha muhimu sana na kinapokosewa madhara yake yanaonekana wazi na kupunguza hadhi ya jengo husika. Lakini ukitembelea eneo la ujenzi na kutathmini kazi yoyote ya ujenzi ukiwa na mtaalamu wa ushauri wa ujenzi ndio utaweza kugundua ni jinsi gani kuna changamoto kubwa katika kufanya kazi kwa usahihi na kwa ubora pale inapokuwa msimamizi mkuu ambaye ni mzoefu na mwenye uwezo wa kutekeleza mradi kwa viwango vya juu kabisa vya ubora na badala yake kuwaachia wasaidizi ambao wengi hukosa uwezo au uzoefu wa utekelezaji wa mradi kwa viwango sahihi. Jambo hili hupelekea baadhi ya vipengele na hatua za ujenzi kwa ujumla kufanyika kwa viwango vya chini visivyoridhisha, na kwa sababu inagharimu sana fedha na muda kurudi tena kufanya marekebisho basi utakuta hali hii huachwa ibaki kama ilivyo hata kama itakuja kuwa wazi kwamba makosa yalifanyika.

MWONGOZO SAHIHI WA UJENZI UTASAIDIA KUKABILI YALE MAENEO YENYE CHANGAMOTO KWA USAHIHI ZAIDI NA KULETA MATOKEO TARAJIWA

Hivyo ili kukabiliana na changamoto hii, kutokana na ukweli kwamba sio rahisi msimamizi mkuu mwenye uwezo mkubwa wa kusimamia utekelezaji kwa viwango vya juu kupatikana katika eneo la ujenzi muda wote, basi anapaswa kutengeneza mwongozo wa kila kitu kitavyofanyika katika kila hatua na namna kila changamoto ambayo inaonekana ni nzito itakavyofanyiwa kazi, sambamba na viwango vya ubora anavyotegemea vifikiwe katika kila kipengele na kuweka mwongozo husika katika maandishi ambao ndio utafuatwa katika utekelezaji. Msimamizi mkuu anaweza kuendelea kufanya marekebisho madogo madogo katika mwongozo huo kila anapotembelea eneo la ujenzi pale anapoona kuna haja hiyo au ikiwa kuna kikao kilikaa na kuamua hivyo ambapo watekelezaji wataendelea kufuata mwongozo huo katika kila hatua kadiri ya namna msimamizi mkuu ameamua. Hii itasaidia pia hata kuwajenga wasaidizi hawa kukua sana kiuwezo kuelekea uwezo wa msaidizi mkuu na uzoefu huu kujengeka kwao kirahisi na kutumia miongozo kama hiyo katika miradi mingine.

MIONGOZO YA MAMLAKA IENDE SAMBAMBA NA MIONGOZO YA WASIMAMIZI WAKUU WA MIRADI HUSIKA KATIKA ENEO LA UJENZI

Kuweka utekelezaji katika mwongozo itampunguzia sana usumbufu msimamizi mkuu na kuokoa muda mwingi wa majadiliano na kila mara kutoa mwongozo kwa mdomo na pia kupunguza sana makosa katika mradi husika wa ujenzi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *