VIVULI VYA MAEGESHO YA MAGARI (CAR SHADES)
Kutokana na mazoea watu wanapofirikia kuhusu maegesho ya magari hufikiria katika mitazamo mikubwa miwili. Ikiwa ni maegesho ya magari nyumbani basi ni aidha kuna eneo la wazi la nje la maegesho ya magari au ni eneo la ndani ya nyumba la kuegesha gari au magari.
Ikiwa ni maegesho ya magari katikati ya mji au maeneo ya umma basi mara nyingi hufikiria ni kwenye maeneo ya wazi au ndani ya jengo maalum kwa ajili ya maegesho ya magari.
Njia zote hizi zina changamoto za aina tofauti, kwa nyumbani kuegesha gari katika eneo la wazi huathiriwa na hali ya hewa ikiwa jua ni kali gari inapigwa sana na jua na kupata joto ambalo huleta hali ya joto ndani ya gari ikiwa unataka kulitumia nyakati za jua, na jua na mvua zikiwa zinalipiga gari baada ya muda mrefu huanza kuharibu muonekano wake kwa kupauka au kupata kutu na michirizi.
Lakini pia njia ya kuweka maegesho ya gari ndani ya nyumba husababisha nyumba kuwa kubwa na kuongeza sana gharama ya ujenzi, na wakati mwingine pia kwa kuwaeneo la maegesho huwa ni kubwa huwezi hata kuathiri muonekano wa jengo.
Kwa maeneo ya katikati ya mji au maeneo ya umma, maegesho ya wazi husababisha huathiri magari kwa kupiga na jua na kusababisha joto sana na pia ikifanyika kwa muda mrefu huathiri muonekano wa gari na kuhitaji ukarabati unaohusisha gharama kubwa.
Kwa maegesho ya gari katika majengo maalum ya kuegesha magari kwa katikati ya miji au kwenye maeneo mengine ya umma hutumia gharama kubwa kujengwa na hivyo pia kuhusisha gharama kubwa katika maegesho haya. Hata hivyo kutokana na thamani ya ardhi na uhaba wake katikati ya miji hasa miji mikubwa huu mbadala wa kujenga majengo makubwa bado unaweza kuwa ndio njia sahihi zaidi.
Maegesho ya magari ya kutumia vivuli vilivyojengwa kwa gharama nafuu maarufu kama “Car Shades” ni chagua sahihi zaidi kwa maeneo yote ya nyumbani na maeneo ya umma. Kwa maeneo ya nyumbani hoja ya usalama wa gari inaondolewa na uwepo wa uzio imara wa ukuta ambao hauruhusu mtu yeyote wala kitu chochote kisichohusika kuona chochote kilichopo au kinachoendelea ndani ua uzio.
Maegesho ya vivuli vya magari yakijengwa kwa usahihi kwa kuzingatia upande wa jua linachomoza na kuzama ni njia rahisi na nafuu zaidi ya kukabiliana na changamoto hizi za maegesho ya magari.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!