FANYA UKARABATI WA NYUMBA YAKO, IKIWA KUNA VITU UNATAMANI VIWEPO.

Kabla mtu hujaanza kuishi kwenye nyumba sio rahisi kuona changamoto zake, ni baada ya kuishi ndani ya nyumba kwa muda na kutumia maeneo yote ya nyumba yako ndio mtu huweza kuona kuna maeneo ungetamani yawe tofauti na yalivyo sasa.

Mara nyingi huwa tunajenga aidha tukiwa bado kuna uzoefu wa vitu vingi hatujakutana nao au wakati kipato chetu bado ni kidogo zaidi au hata wakati familia bado ni ndogo zaidi, lakini baada ya muda hujikuta tunabadili mawazo na kufikiri kwamba kuna vitu vya ziada tungehitaji kuwa navyo.

UKARABATI WA NYUMBA KUIONGEZA KUWA GHOROFA

Lakini kwa kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kipato au mazoea watu wengi hawapendi kuanza ujenzi mpya ambao unaendana na mahitaji yake mapya na kuhamia kwenye makazi haya mapya, lakini bado akiw ana uhitaji mkubwa na wa lazima wa kuboresha nyumba yake kwa namna anayohitaji.

Hivyo suluhisho hapa ni kufanya ukarabati wa nyumba yako iendane na mahitaji yako ya sasa, suala ambalo linawezekana kabisa iwe na kuongeza ukubwa wa nyumba yako au hata kuongeza sakafu nyingine juu yake na kuifanya kuwa ghorofa.

Au ikiwa unahitaji kuiboresha kwa kuongeza matumizi zaidi ya ndani bado ni suala linalowezekana vizuri sana, hivyo kwa kuwa uhitaji umeongezeka na kipato pia kimeongezeka ni muhimu sana mtu kuchukua hatua hii muhimu ambayo inakidhi mahitaji yako ya sasa kwani kwa wakati unajenga hayakuwa muhimu.

UKARABATI WA NYUMBA KUIONGEZA KUWA KUBWA ZAIDI KUTOKANA NA KUKUA KWA MAHITAJI

Ni suala la kawaida katika kila eneo la maisha kwa mahitaji ya mtu kuongezeka kadiri muda na umri unavyoongezeka kwa sababu mtu hubadilika, mazingira hubadilika, kipato hubadilika na hata familia huongezeka, hivyo mahitaji nayo ni lazima yatabadilika na kuongezeka.

Suala la ukarabati ni suala muhimu sana lakini hiyo ni sehemu muhimu zaidi ya kuhakikisha utaalamu unahusika kuliko sehemu nyingine yoyote na ni muhimu zaidi kumshirikisha kwanza mtaalamu ukapata mchango wa mawazo na ushauri ili kuona uhalisia wa kile unachokihitaji.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *