KAZI YA UJENZI KATIKA HATUA YA “FINISHING”.

Japo ubora wa kazi ya ujenzi huhitaji umakini mkubwa tangu mwanzoni kabisa wa kazi husika na pia kazi ambayo haikujengwa kwa usahihi tangu mwanzoni madhara yake huendelea kuonekana mpaka mwishoni mwa kazi lakini hatua ya “finishing” huhitaji umakini mkubwa wa ziada kwa sababu ndio hubeba taswira ya mwisho ya nyumba.

Licha ya kwamba gharama ya “finishing” ya jengo kwa wastani ni sawa na gharama ya hatua yote ya awali ya ujenzi kabla ya “finishing” lakini mwenendo wa matumizi ya fedha hasa kwa watu wasio na uzoefu mara nyingi huenda vibaya na kugharimu sana hatua ya “finishing” ambayo kupungukiwa kwa fedha kutokana na usimamizi wa fedha usio sahihi hupelekea kazi ya “finishing” kudorora na kushindwa kufikia viwango sahihi vya ubora vilitarajiwa.

Kazi ya ujenzi katika hatua ya “finishing” ili iweze kufanyika kwa viwango sahihi kwanza inahitaji kazi iliyotangulia ya kuanzia msingi mpaka kupaua iwe ilifanyika kwa usahihi, pili inahitaji usimamizi mzuri wa fedha za mradi kwa usahihi kwa kuzingatia uzito na ugumu uliopo kwenye kazi ya “finishing” na tatu ni ufundi sahihi na usimamizi sahihi wa kazi nzima ya “finishing” katika kufanikisha kile kinachoazimiwa.

Kushindwa kuzingatia mambo hayo matatu muhimu katika kazi ya ujenzi kwa ujumla hupelekea kazi ya “finishing” ya jengo kufanyika kwa viwango visivyoridhisha na kusababisha taswira duni ya jengo licha ya kwamba gharama za ujenzi husika kuwa kubwa hasa kwa upande wa malighafi/”materials”.

Karibu sana kwa kazi bora za ujenzi kwa hatua zote kwa viwango vinavyotarajiwa.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *