UBORA WA MUONEKANO WA JENGO KATIKA PICHA NI MWONGOZO WA UBORA KATIKA UHALISIA.

Katika kazi ya usanifu wa jengo maarufu kama kuchora ramani ya jengo huwa kwa kawaida inahusisha hatua tatu kubwa. Baada ya kukusanya taarifa zote za kiwanja pamoja na mahitaji ya mteja kazi ya usanifu wa jengo hufuatiwa na hatua tatu mpaka kukamilika ambazo ni hatua ya kutengeneza wazo(concept stage), hatua ya kutengeneza muonekano wa nje ikiwa ni pamoja na paa(3D’s design stage) na hatua ya kutengeneza michoro ya mwisho yenye taarifa zote muhimu(final detailing stage).

Katika hatua hizi tatu hatua ya pili ndio hatua ya kutengeneza muonekano wa nje wa jengo pamoja na paa ambao nao unatokana na hatua ya kwanza ya wazo na msingi wa usanifu wa jengo.

Ubora wa kazi ya usanifu wa hatua hii ya pili ambao ndio mfano wa jengo lenyewe katika muonekano wa picha wa namna linakwenda kuwa katika uhalisia baada ya kumalizika kujenga huwa ni mwongozo mzuri na sahihi sana katika kuhakikisha matokeo tarajiwa yanafikiwa katika viwango vinavyoonekana.

Kisaikolojia mwongozo wa mfano halisi wa kitu unapokuwepo moja kwa moja watu hufikiria namna ya kufanikisha kitu husika kwa kadiri mwongozo huo unavyoonyesha ambapo ikiwa watashindwa kufikia yale matarajio kama yalivyo katika mwongozo watajiona wameshindwa.

Lakini pia mwongozo huo hurahisisha kazi husika ya ujenzi kwani kila kitu huwa tayari kimeonekana katika picha kwenye matokeo ya mwisho na hivyo kinachokuwa kinafanyika ni kutafuta aina zote za nyenzo za kuhakikisha matokeo husika yanafikiwa.

Hivyo uzito wa kazi ya usanifu wa jengo ambao unajumuisha hatua zote tatu muhimu unapaswa kupewa kipaumbele kwa sababu ndio unaoamua hata ubora wa matokeo ya mwisho kabisa ya ujenzi wa jengo husika.

Karibu tukuhudumie.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *