NYUMBA NYINGI ZINAJENGWA CHINI YA KIWANGO
Moja kati ya mambo muhimu ambayo bado hayapewa uzito unaostahili uelewa wa viwango mbalimbali vya huduma za ujenzi. Kazi nyingi za ujenzi hufanyika lakini hakuna mfumo wa kupima viwango vya ubora vya kazi husika na kuleta mrejesho ambao kwa kutumia vigezo fulani utasaidia kuweka madaraja mbalimbali ya viwango vya yatakayohamasisha ubora zaidi wa kazi.
Suala hili limepelekea kazi nyingi za ujenzi kufanyika chini ya viwango na kwa kuwa hakuna uelewa mkubwa wa viwango vya ubora, watu hawajishughulishi sana na kuboresha kazi.
Hii imekuwa changamoto zaidi kwa wale wanaojitahidi kufanya kazi kwa viwango vya juu kwa kutoa thamani kubwa ambayo kwa bahati mbaya imekuwa haithaminiwi na kulipwa zaidi kwa kufananishwa na wengine wasiofanya kazi kwa viwango kwenye suala la bei na kupelekea ubora kwa ujumla kuzidi kushuka.
Kwa uzoefu wangu binafsi kazi nyingi ambazo nimekuwa nikizitembelea au kupewa kazi ya kufuatilia ubora wake huwa nakuta zikiwa zimefanyika chini ya viwango na kuambatana na makosa mengi kutokana na changamoto ya usimamizi.
Hivyo ni muhimu sana mtu unapofikiria kujenga nyumba yako ufikirie ubora wake katika maeneo yote muhimu kuanzia umahiri wa kiufundi uimara wa jengo n ahata mpangilio sahihi na hivyo kuweka umakini mkubwa kwenye kuchagua watu sahihi wa kufanya nao kazi.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!