UTAALAMU, USIMAMIZI NA MAKUBALIANO MAALUM VITAKUHAKIKISHIA UBORA.

Tumejifunza kwamba kazi nyingi za ujenzi zinafanyika chini ya kiwango kutokana na kukosekana kwa uelewa wa viwango vya ubora vya kazi za ujenzi kwa sababu ya watu kutojali na kutotambua thamani ya tofauti inayotolewa na watu tofauti.

Hata hivyo jambo la kwanza na muhimu sana katika kuhakikisha ubora na kutumia huduma za kitaalamu za ujenzi kupata michoro ya ramani ambayo ndio itatoa mwongozo sahihi wa ubora huo, kisha kuweka usimamizi madhubuti wa kuhakikisha mwongozo huo unafuatwa kwa uhakika kadiri ilivyokusudiwa.

Katika kuhakikisha kwamba viwango sahihi vya ubora vinakuwepo kunatakiwa kufikiwa kwa makubaliano maalum kwa pande zote ambayo yatapelekea uwajibikaji wa pande zote mbili na hivyo yale yanayoazimiwa yanafikiwa kadiri ya makubakiano.

Mpango rahisi na wa uhakika kama huu utasaidia sana kuhakikisha thamani ya fedha inayotolewa inaendana na ubora wa thamani ya huduma husika kwa faida ya pande zote mbili. Ushirikiano na uwajibikaji wa namna hii utapelekea matokea bora na mahusiano bora zaidi za kikazi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *