GHARAMA ZA HUDUMA ZA UJENZI ZINATOFAUTIANA KATI YA MTAALAMU MMOJA NA MWINGINE.

Huduma za kitaalamu katika ujenzi ni kama ilivyo biashara ya huduma au bidhaa nyingine yoyote katika soko, kwamba bei za huduma na bidhaa hizo hutofautiana kwa sababu mbalimbali. Utofauti wa bei kwa huduma na bidhaa katika soko ni kitu cha kawaida na hilo huchangiwa na sababu mbalimbali hususan utofauti katika viwango vya ubora wa huduma na bidhaa hiyo.

Kama ilivyo kwa biashara nyingine kwenye biashara ya huduma za ujenzi hili limekuwa ni jambo gumu kidogo kwa baadhi ya watu wasio na uelewa mpana wa ujenzi pamoja na utofauti wa gharama kwa kadiri ya ubora wa huduma ya ujenzi husika wamekuwa wakifikiria kwa mtazamo wa usawa wa bei. Nafikiri jambo la muhimu sana la kuzingatia ni ubora wa huduma zaidi kuliko usawa wa bei.

Imekuwa kawaida kwenye huduma za ujenzi pale mteja anapohitaji kuambiwa gharama za huduma fulani ya ujenzi na baada ya kufahamu anasema ni gharama kubwa kwa sababu kuna sehemu nyingine aliyoambiwa kwamba anasema kufanyiwa kwa gharama ndogo zaidi ya hiyo, bila hata kujua bayana utofauti ni watoa huduma hao wawili na matokeo anayokwenda kuyapata.

Mara nyingi utakuta kwamba huduma inayotolewa ni ya viwango duni na idadi vipengele vinavyojumuishwa ni vichache na pengine kazi hiyo inaweza kuwa na mapungufu mengi kwa mhusika kukosa uzoefu wa kazi kwa kutofanya kazi nyingi vya kutosha. Hata hivyo sio kwamba mara zote huduma ya bei rahisi inamaanisha ni huduma ya viwango duni lakini huwa ni mara chache kuwa kinyume chake na hiyo inatokana na sheria ya asili ya uhaba na utele.

Sheria ya uhaba na utele iko kwamba mtu anapokuwa na uhaba anakuwa tayari kupunguza sana masharti na kukubali hata kidogo kinachoweza kupatikana lakini mtu anapokuwa na utele anabaki katika viwango vyake bila kushuka kabisa. Sasa mtu anaweza kuwa na uhaba kwa sababu kadhaa kwanza inawezekana kwamba bado hajawa na uzoefu mkubwa na uwezo mkubwa ndio maana anapata kazi chache au anaweza kuwa hafanyi kazi za viwango sahihi hivyo anajikuta muda mwingi hana kazi na hivyo ana uhaba.

Mtu mwenye utele mara nyingi utakuta anafanya kazi za viwango vya juu na hivyo anadai fedha inayoendana na viwango hivyo na kulipwa vizuri hivyo anakuwa hayupo sana kwenye uhaba au anakuwa anafanya kazi nzuri hivyo analetewa kazi nyingi na hivyo kujikuta yupo kwenye utele na hashushi viwango vyake vya ubora wala malipo kwa sababu anajua wazi kwamba akianza kushusha kiasi cha malipo moja kwa moja atajikuta pia anashusha viwango vyake vya ubora na hivyo kuanza kupotea.

Kitu kikubwa kinachomlinda na kumfanya aendelee kuwa juu ni viwango vyake vya juu vya ubora wa kazi anazofanya na gharama anayotoza na mara atakapoanza kushusha viwango vyake ndipo atakapopotea kwenye kazi. Hivyo inakuwa sio sawa au ni makosa kumtumia kigezo kwamba mbona kuna mwingine anafanya kwa gharama za chini zaidi hasa pale unapokuta hufahamu kwa usahihi utofauti wa viwango vya kazi za watu hao tofauti kwa mtazamo rahisi na hata kwa mtazamo tata.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *