HUDUMA ZA UJENZI ZA BURE HAZINA THAMANI.
Ni kanuni ya asili kwamba vitu vinavyoweza kupatikana bure au hata kupatikana kwa urahisi sana basi thamni yake ni ndogo sana na wakati mwingine havina thamani kabisa. Hii ni kanuni ya asili ambayo sio tu kwamba nimejifunza kwenye nadharia ya vitabu bali imenitokea mara kadhaa kwenye kazi zangu za kila siku na hasa katika shughuli za ujenzi.
Haijalishi kitu ni muhimu kiasi gani kanuni ya asili ni kwamba kama kinaweza kupatikana bure au kwa urahisi sana basi thamani yake pia huwa ni ndogo sana hata kama ni kitu kizuri sana au kina umuhimu mkubwa sana. Angalia tu hata mfano wa vitu muhimu kama hewa tunayovuta, ni muhimu sana na ndio uhai wenyewe lakini inapatikana bure na sio rahisi mtu kukubali mtu yeyote akuuzie tofauti na madini kama dhahabu ambayo hayana umuhimu wowote kwenye maisha yako lakini kwa kuwa hayapatikani kiurahisi gharama yake ni kubwa sana licha ya kutokuwa na umuhimu kama ilivyo hewa ya oksijeni.
Wakati nimeanza kufanya kazi za kutoa ushauri wa kitaalamu kwenye ujenzi miaka michache nyuma baada ya kumaliza chuo Rafiki zangu wengi ambao nilisoma nao na wengine ndugu zangu waliomba niwafanyie kazi zao na kama jinsi ilivyokuwa ni ndugu na Rafiki wa karibu niliwafanyia kazi hizo bure kabisa bila kuwatoza kiasi chochote cha malipo kwa huduma hiyo.
Ajabu ni kwamba katika wote niliowafanyia kazi bure hakuna aliyejali wala kuthamini kazi hizo na mbaya zaidi wala hawakuzijenga zaidi waliona kama pengine zina mapungufu na kufikiria zaidi labda wanaweza kuziboresha kidogo, lakini isipokuwa kama wawili ambao kweli walienda kuzijenga lakini ajabu ni kwamba wale walioenda kujenga walikuja kunilipa pesa kiasi kwa huduma ile kwa sababu.
Jambo hili japo nilikuwa nimejifunza kutoka kwenye nadharia za vitabu lakini nilikuja kupata Ushahidi wake katika uhalisia kupitia watu wa karibu kabisa na hapo ndipo nilipoongeza umakini sana kwenye huduma zozote za bure na hata zile za gharama ndogo sana isiyolingana na thamani ya huduma husika.
Hii ndio kwa sababu leo hii mtu anapojitokeza na kutoka nimfanyie kazi yake bure au kwa gharama ya chini sana isiyolingana na thamani ya huduma hiyo huwa naanza kufikiria kama mtu huyo kweli yuko “serious” na kazi hiyo hiyo kiasi gani kwa sababu kutoka kwenye uzoefu nimejifunza sana kuangalia mtazamo wa mtu kwa kile anachokithamini kiasi cha kukipa gharama inayostahili na kile asichokithamini na karibu mara zote majibu huwa ni hayo hayo.
Hivyo nilijikuta naongeza umuhimu sana kwenye kushughulika na watu ambao nawaona kabisa kwamba wanathamini kile wanachokihitaji kwani kwa njia hiyo ndio pia wanaweza kuthamini huduma unayowapatia na kukuthamini mtoa huduma pia kuwa kuhakikisha wanalipa gharama inayolingana na thamani wanayokwenda kuipata.
Karibu sana tukuhudumie kwa thamani inayokustahili.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!