IKIWA UNATHAMINI UBORA KWENYE UJENZI, WEKEZA KWENYE USHAURI WA KITAALAMU.

Katika kufanya jambo lolote ni muhimu kufahamu sehemu ambayo inaleta matokeo muhimu zaidi ambayo unahitaji kuweka nguvu kubwa zaidi au umakini wa hali ya juu zaidi. Watu wengi wanapofikiria kuhusu ujenzi, japo kiuhalisia mwisho wa siku huwa wanahitaji sana ubora lakini huwa wakati wanafikiria kuhusu ujenzi hawafikirii sehemu sahihi ya kuweka nguvu na umakini zaidi ili kufikia ubora ambao wanauhitaji iwe wanajua au hawajui.

Mchakato mzima wa ujenzi kuanzia mwanzo kabisa wakati wa kuanza kutengeneza michoro ya ramani mpaka kukamilisha ujenzi na kuhamia kuna vipengele vingi sana vya kuzingatia lakini ili kupata ubora na matokeo unayotamani mwishoni wa siku kuna maeneo au vipengele ambavyo utatakiwa kuvipa kipaumbele zaidi ili kufanikisha kile unachotaka.

Changamoto ni kwamba watu wengi wanapofikiria kuhusu ujenzi huwa hawapeleki akili zao kwenye maeneo au vipengele vitakavyoamua matokeo haswa yale wanayotazamia bali hupeleka akili zao kwenye maeneo mengine ya mchakato yanayoonekana kiurahisi kwa nje lakini yakiwa hayana madhara makubwa katika shughuli nzima inayokwenda kuamua thamani au ubora wa jengo lenyewe.

Katika ujenzi sehemu ya kwanza na muhimu sana inayokwenda kuamua na kulazimisha matokeo haswa yale ambayo mwisho wa siku unayatazamia ni eneo la ushauri wa kitaalamu kuanzia mwanzoni wakati wa kuandaa michoro ya ramani mpaka kwenye hatua ya usimamizi wa kazi yenyewe. Msisitizo unapowekwa kwenye maeneo hayo mawili yaani kuandaa michoro na usimamizi sahihi basi matokeo yanayotarajiwa lazima yatafikiwa.

Shida inakuja kwamba watu wengi badala ya kupeleka nguvu na umakini katika maeneo haya wanaamua kupeleka katika maeneo mengine na kupuuza haya kama vile kununua malighafi za bei ghali, au kushughulika na mafundi ambao hajui namna sahihi ya kushughulika nao. Usimamizi wa matokeo bora ni sayansi na sanaa ambayo mtu anaijifunza kwa muda mrefu wa kuifanya mpaka anapokuwa na uhodari mkubwa katika utekelezaji tofauti na mtu ambaye hana uzoefu nayo kabisa.

Hivyo kupitia kufahamu sehemu sahihi za kuweka nguvu ili kufanikisha matokeo unayotamani ni muhimu katika kuokoa muda na kufanikiwa kupata thamani kubwa inayolingana na gharama unayokwenda kuwekeza hapo.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *