RAMANI ZA NYUMBA ZA KISASA ZINA THAMANI INAYOKUSTAHILI.

Gharama ya kujenga nyumba ya kuishi sehemu yoyote ile inahusisha gharama kubwa sana mpaka kukamilika. Hii ni kwa sababu kuna vitu vingi katika ujenzi kwa upande wa vifaa na hata ufundi ambavyo havina mbadala wa kupatikana kwa gharama ya chini zaidi ya wastani ambao upo kwenye soko hivyo hakuna namna yoyote mtu unaweza kupita ukaacha kuingia gharama kubwa katika ujenzi.

Lakini ni hasara na maamuzi yasiyo sahihi kuamua kutumia fedha nyingi katika ujenzi pasipo kuwa na mwongozo wa kitaalamu ambao utasaidia kuleta matokeo bora na ambayo utajivunia kwa sababu ya gharama kubwa ambayo mtu unaingia. Kazi inayojengwa inapokosa kuwa na mwongozo wa kitaalamu ambao umefanyika kwa viwango sahihi ni kazi inayofanyika kwa makosa ya uzembe.

Kwa sababu gharama kubwa unayoenda kuiweka kwenye ujenzi inaposhindwa kuleta matokeo bora na ya kutamanika kwa sababu ya kukwepa gharama ya kupata mwongozo wa kitaalamu wa michoro sahihi iliyofanyika kwa viwango sahihi ni makosa ya kijinga na uzembe. Unapofikiria kujenga nyumba ya kisasa unatakiwa uanze kufikiria kwamba unastahili michoro ya ramani ya kisasa ambayo inaendana na hadhi ya nyumba yenyewe.

Ni makosa makubwa na uzembe wa hali ya juu wa kushindwa kufikiria kwa usahihi pale ambapo mtu unataka kuweka mamilioni kwenye mradi wa nyumba yako ya kuishi ambao unaenda kufanyika kwa namna ambayo haitakuridhisha wala kukufurahisha na pengine haiendani hata na mahitaji yako lakini kutokana na kwamba ulikuwa unajaribu kuruka hatua muhimu sana kwa kufikiri unakwepa gharama ambayo ni ndogo sana ukilinganisha na thamani ya mradi husika unaishia kwenye kazi ya viwango duni.

Ramani za nyumba za kisasa zina thamani inayokustahili bila kujali unajenga wapi na unajenga kwa muda gani au kwa ukubwa gani, usikubali kujihujumu kiasi hicho na kuishia kujilaumu baadaye, fanya maamuzi sahihi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *