KWENYE UJENZI KILA KITU KINA GHARAMA YAKE.

Kuna changamoto kubwa kwenye ujenzi kwa watu kuwa mabadiliko au vitu vya tofauti wanavyokuwa wanavitaka bila kufikiria gharama inayokuja na mabadiliko hayo au vitu hivyo. Ni kawaida inatokea mtu kutaka kufahamu gharama ya ujenzi na kuambiwa halafu kama kujadili mradi wenyewe kwa marefu na mapana akahitaji vitu vinngi sana vya ziada bila kufikiria kama vitaathiri bei iliyotajwa au la.

Ukweli ni kwamba mtu anapokadiriwa gharama za ujenzi wa mradi fulani huwa anakadiriwa kwa mazingatio fulani lakini mradi huo unapokwenda nje ya mazingatio yaliyofikiriwa gharama yake inaanza kuongeza kujumuisha yale ambayo hayakudhaniwa katika mazingatio yaliyowekwa, hii ni kwa sababu kila kinachoongezeka nje ya mazingatio yaliyowekwa kinaongeza gharama zaidi.

Ni muhimu sana pale ambapo gharama ya ujenzi inapokadiriwa kwa ajili ya mteja kufanya maamuzi ijadiliwa kwa kina na kujua mazingatio yaliyowekwa yanavyojumuisha na kama kuna vitu vimetajwa visivyojumuishwa katika makadirio ijulikane kwamba gharama inaenda nje ya bajeti ya makadirio ya gharama yaliyofanyika.

Hili litasaidi kupunguza sintofahamu lakini pia litampa mteja fursa ya kuamua kwa usahihi ni yapi anayofikiri ni muhimu zaidi na yapi sio muhimu ikiwa anahitaji kupunguza gharama za ujenzi wa mradi huo.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *